Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano Samia Suluhu Hasani AENDELEA NA ZIARA YAKE HUKO PEMBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano Samia Suluhu Hasani AENDELEA NA ZIARA YAKE HUKO PEMBA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano Samia Suluhu Hasani akipata Maelezo kutoka kwa Afisa Mdhamini wa Wizara ya Mfugo na Uvuvi Bi Mayasa Hamad  Ali alipotembelea Jengo jipya la Wizara ya Wifugo na Uvuvi Pemba lilojengwa kwa ufadhili wa Macemp
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makomo wa Rais Muungano Samia Suluhu Hasani akipata Maelekzo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa Maradi wa barabara  ya mzambarau takau finya kisiwani pemba bw rakesh malok unaodhaliwa na MCC .
waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hasani akipata Maelezo  Kutoka kwa katibu wa Baraza la mji wa wete Bw Hamad Khamis Hamad katika chinjio la ngombe liopo wete  kiwani pemba wete ambalo limakarabatiwa kwa ufadhili wa mfuko wa maendeleo ya jimbo CDCF.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makomu wa Rais Muungano Samia Saluhu Hasani akitembelea Jengo la Ikulu ya Wete Pemba, ambayo ni Ikulu ya Makomu  wa Rais Kiwani Pemba baada ya kufanyiwa matengenzo ya awali.Picha na Ali Meja
---
Waziri wa nchi ofisi  ya makamu wa rais muungano amewataka wananchi kutoita majina ya wafadhili miradi ya maendeleo ili kuonyesha uzalendo na kuwa na uchungu nayo .
Ameyasema hayo wakati akikagua jengo la wizara ya mifugo na uvuvi pemba ambalo limejengwa kwa ufadhili wa macep ,ili kutoa huduma kwa umakini za wazara hiyo .
Akizungumza kwa ufasaha amesema  kuwa kazi ya  wafadhili  ni kutoa fedha tu lakini suala la  utunzaji wa maradi ni jukumu letu sisi ambao ndio walengwa wakuu wa miradi hiyo ya maendeleo.

Akisisitiza juu ya suala hilo mbalo limekuwa ni moja ya mambo makubwa yanayotukabili katika miradi mbali mbali kwa sasa ,Hivyo sasa ni wakati  wananchi wahusika kuipa majina yao wenyewe ili miradi hiyo iwe na tija kubwa kwa jamii husika .

“Utasikia mtu anasema mradi wa macep mara, assp ,who, au unicef ,lakini kama hili jengo lenu linatwa jadari house kwa maana yake hasa ili kutoa chachu ya kuwa na imani na miradi mbayo walengwa wake wakuu ni wananchi husika .

Alisema waziri Samia kwa msisitizo  “sasa kazi  iwe kwanu namna ya kulitunza na kulindesha kwa utaratibu mzuri na salama “ alisema waziri samia.

Leo waziri samia akiwa ni siku yake ya pili katika ziara hapa kisiwani pemba  amefanya ziara ya kuikagua Ikulu ya wete ambayo ndio lkulu ya makamu wa rais pemba  .
Pia  samia na ujumbe wake walipitia katika chinjio la ngo,mbe la wete ambalo limefadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jimbo unaotokana na bunge la jumuhuri uya mungano  (CDCF) ambao ni mfuko wa mandeleo   jimbo na kujionea hali ilivyo katika eneo hilo ,wakati mchana alitembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa barara zaidi ya kilomita 35  katika kisiwa cha pemba unajegwa kwa ufadhili wa mradi mcc kutoka mbamabarau takau hadi finya .

Wakati akiwa katika zira hiyo alipata furusa ya kutembelea ofisi za wa wabunge katika majimbo ya micheweni na mchangamdogo  ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa bunge la jumuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mfuko wa maendeleo .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages