Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda(kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari la huduma ya mkoba (mobile clinics) Dk. Noah Chihoma kutoka Hopitali ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
Meneja
Mkuu wa kutoka Ship Building& Repair, Darryl Lain akitoa maelekezo
kwa baadhi ya wawakkilishi wa hospitali zilizopewa magari hayo jinsi ya
kutumia gari la huduma ya mkoba(mobile clinics).
Baadhi
ya watumishi wa afya wakiwemo waandishi wa habari wakimwangalia Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda wakati akiendesha mmoja ya
gari ya huduma ya mkoba(mobile clinics)
--
NA MAGRETH KINABO – MAELEZ0
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa magari saba ya huduma za mkoba kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wengi kupata huduma za madaktari bingwa hususan walioko vijijini.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda wakati
akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi magari hayo kwa
wawakilishi wa hospitali mbalimbali kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara
hiyo.
“Tunagawa magari haya kwa madhumuni ya kupeleka huduma za wataalamu bingwa karibu na wananchi.
“Lengo
la Serikali ya Awamu ya Nne ni kuhakikisha huduma za afya na ustawi wa
jamii zinawafikia nchinii kote na hasa vijijini, ambako ndipo wanapoishi
wananchi wengi. Haya magari yatatumiwa na madaktari bingwa katika kanda
zetu zote nchini kote,” alisema Waziri Mponda.
Aliitaja
thamani ya magari hayo kuwa ni sh. milioni 181 kwa kila mmoja ambayo
inahusisha pamoja na vifaa vilivyoko ndani ya gari.
Waziri
Mponda aliongeza kuwa watumishi kutoka hospitali husika watafundishwa
namna ya kutumia magari hayo ambayo yana vifaa maalaum vipya vya kisasa,
ambao watawaelekeza wenzao wakati wa kliniki hiyo.
Alivitaja
vifaa hivyo kuwa ni vya kufanyia uchunguzi na vya kutolea huduma.
Magari hayo pia yana jenereta kwa ajili ya kupata umeme sehemu ambazo
hazitakuwa na umeme.
Hospitali zilizopata magari hayo za Kanda ya Mashariki ni CCBRT Dares Salaam, Kasikazini KCMC Kilimanjaro, Kati Chuo Kikuu cha Dodoma Kusini Rufaa ya Mbeya, Kusini Mashariki Ndanda Mtwara, Magharibi Maweni Kigoma na Ziwa Bugando.
Wakizungumzia kuhusu magari hayo wawakilishi wa hospitali hizo walisema wanaishukuru serikali kwa kuwa utawezesha wananchi wasioweza kufikia huduma za afya kuzipata kwa kiurahisi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)