Waziri Kawambwa atembelea Chuo Kikuu Ardhi HAPO JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Waziri Kawambwa atembelea Chuo Kikuu Ardhi HAPO JANA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) akifafanua jambo wakati wa akijibu maswali kutoka kwa watumishi na wanafunzi wa chuo hicho mara baada ya kufanya ziara katika Chuo Kikuu Ardhi Dar es Salaam kwa ziara ya Mafunzo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro na aliekaa kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Mipango, Fedha na Utawala Prof. Eliutha Mwageni
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam kwa ziara ya Mafunzo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Idrissa Mshoro na aliekaa kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Mipango, Fedha na Utawala Prof. Eliutha Mwageni
Makamu Mkuu Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akimweleza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) mitambo mbalimbali inayotumika kutengeneza Ramani za miji kupitia picha za anga na satellite. Waziri Kawambwa alifanya ziara ya mafunzo chuoni hapo jana kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za Chuo hicho
Dk Evaristo Liwa, Mkuu wa Kitengo cha Geospatial Science katika Chuo Kikuu Ardhi akimwonesha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) mitambo mbalimbali inayotumika kufundishia wanafunzi chuoni hapo. Kushoto ni Makamu Mkuu Chuo Kikuu Ardhi Prof. Idrissa Mshoro
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa (Mb) (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro, (kulia) Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Mipango, Fedha na Utawala Prof. Eliutha Mwageni (Kushoto ) na baadhi ya watumishi wa Chuo Kikuu Ardhi. Picha zote na Hadija Maulid na Mary Kigosi wa Chuo Kikuu Ardhi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages