Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akikagua moja ya mitaro iliyojengwa na wananchi kwa ajili ya kuhifadhi
vyanzo vya maji kuboresha kilimo cha umwagiliaji, Wilayani Rungwe hivi
karibuni.
************************************
NA MAGRETH - KINABO – MAELEZO
NAIBU
Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, ametoa changamoto kwa
wazalishaji wa chakula nchini kuhakikisha kuwa wanatumia njia sahihi
za kilimo cha kitaalamu ili kuweza kuepusha upungufu wa maji na
uchafuzi wa vyanzo vyake.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri huyo wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya 24
ya wiki ya maji yatakayoanza rasmi Machi 16 hadi 22 mwaka huu.
“Juhudi
za pamoja zinahitajika kati ya wazalishaji wa chakula na wasimamizi wa
vyanzo vya maji katika kuhakikisha kuwa usimamizi bora wa vyanzo vya
maji hususan katika shughuli za kilimo ili nchi yetu iweze kuwa na
uhakika wa chakula,” alisema Waziri Lwenge huku akisisitiza kwamba ‘maji
ni uhai kwa kila kiumbe bila maji hakuna chakula,’ alisema Waziri
Lwenge.
Alisema
kauli mbiu ya maadhimisho hayo, ambayo kitaifa yatafanyika mkoani
Iringa kuwa ni ‘Maji na Uhakika wa Chakula,’. Maadhimisho hayo
yatafanyika kila mkoa na wilaya nchini.
Aliongeza
kuwa mujibu wa takwimu za Shirika la Chakula Duniani(FAO) zinaonyesha
kuwa uzalishaji wa chakula duniani umeongezeka kutoka ka kilimo cha
umwagiliaji lakini asilimia 15(sawa watu 854milioni) wanakabiliwa na
upungufu wa chakula.
Waziri
Lwenge alisema kuna umuhimu wa kuongeza kilimo cha umwagiliaji ili
kuweza kukidhi uzalishaji wa chakula kitakachoweza kukidhi watu bilioni
2.7 katika kipindi cha miaka 50 ijayo.
Katika
maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika ambazo ni utoaji wa
elimu, semina, maonesho ya bidhaa, uwekaji wa mawe ya msingi katika
miradi, mikutano ya hadhara, usafi na michezo, ambapo aliwataka wananchi
kujitokeza kwa wingi.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)