Mwanafunzi
Kelvin Bosco (mlemavu wa akili) toka Shule ya Msingi Naurei wilayani
Arumeru akiandika ubaoni baada ya kupewa maelekezo
Mratibu wa vikundi vya Pambazuko Klabu wilayani Arumeru, Bi. Vick Kimaro..JPG
Mwalimu Philipo Meli wa Shule ya Sekondari Kimyak wilayani Arumeru.

Wanafunzi wenye ulemavu wa Chuo cha Mafunzo kwa Watu wenye Ulemavu Usa River wilayani Arumeru wakifanya mahojiano
--
Na Joachim Mushi,
BAADHI
ya waenezi wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu na wafanyakazi
walemavu wilayani hapa wameitaka Serikali kuonesha kwa vitendo
utekelezwaji wa madhiriano ya mkataba huo ili kundi hilo kuanza kupata
haki sawa za kimsingi kama ilivyo kwa watu wa kawaida.
Changamoto
hiyo imetolewa hivi karibuni na Bi. Vick Kimaro ambaye ni mmoja wa
viongozi wawakilishi wa watu wenye ulemavu wilayani Arumeru, wanaofanya
kazi kwa ushirikiano na Kituo cha Habari Kuhusu Walemavu (ICD) cha
jijini Dar es Salaam.
Bi.
Kimaro ambaye ni mlemavu wa viungo (mguu) alisema licha ya Serikali
kuridhia utekelezaji wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu bado
maeneo mengi, baadhi ya wananchi na hata viongozi hawatambui uwepo wa
mkataba huo, ikiwa ni pamoja na kutojali haki za msingi kwa walemavu.
Alisema
kutokana na hali hiyo bado watu wenye ulemavu wamekuwa wakikumbana na
vikwazo vingi katika ufuatiliaji wa haki mbalimbali ambazo ni za msingi
kwa jamii yote.
“...unaweza
kujiuliza kama tayari kuna mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu ambao
Serikali imeridhia kwanini tunaendelea kukubwa na vikwazo kwenye huduma
anuai za msingi?,” alisema Bi. Kimaro.
“Pia
huwezi kuamini hadi leo wapo baadhi ya viongozi ambao hawatambui
chochote juu ya ujio wa mkataba huo na ndiyo maana wanashindwa
kuusimamia katika ngazi zao,” alisema Bi. Kimaro ambaye ni Mwakilishi wa
Watu wenye Ulemavu wa Chama cha Walimu Arumeru.
Akizungumza
katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Philipo Meli ambaye ni
mwalimu mlemavu (asiyeona) wa Shule ya Sekondari Kimyak wilayani Arumeru
amesema Serikali ndiyo inayopaswa kuonesha njia ya kuwajali walemavu
hasa katika elimu.
Alisema
bado nyenzo za kufundishia na kujifunzia kwa watu wenye ulemavu
hazipewi kipaumbele jambo ambalo linaweza kuwadidimiza kundi hilo katika
harakati ya kujikomboa na hata kujitegemea.
“Mimi
ni mwalimu mlemavu wa macho nafundisha kwa kutumia nyenzo maalumu
lakini nyenzo hizo sina...kitu cha msingi ambacho Serikali inatakiwa
kukikazania kwa kundi hili ni kuwapa elimu kama ilivyo kwa makundi
mengine. Binafsi nimetembelea kiwanda cha vitabu pale Dar es Salaam juzi
hakuna vitabu kabisa vya walemavu, sasa utamsaidiaje mlemavu kwa mtindo
huu...,” alisema Meli akizungumza kijijini Kimyak.
Alisema
mara zote anapofuata vitabu kwa ajili ya kufundishia hapati vyote na
hata vilivyopo vimepitwa na wakati jambo ambalo ni gumu kuwasaidia watu
wenye ulemavu. “Kiwanda hiki ndicho kinachochapisha vitabu kwa watu
wenyeulemavu...wanasema hawana vitabu kwa kuwa hawapati ruzuku ya
kutosha serikalini, yaani kati ya vitabu 86, ambavyo vinahitajika kwa
kada hii ni vitabu sita tu nilipewa nilipofuatilia nyenzo hizo Dar es
Salaam, kwa hali hii utamsaidiaje mlemavu.
Aidha
alisema elimu ndio nguzo ambayo Serikali inapaswa kuiongezea nguvu
kwani iwapo idadi kubwa ya kundi hili litawezeshwa kielimu linaweza
kufanya mabadiliko na kujikomboa kiuwezo kabla ya kuingia katika huduma
nyingine.
'Habari hii imeandaliwa na mtandao wa Thehabari.com www.thehabari.com kwa kushirikiana na Kituo cha Habari Kuhusu Ulemavu (ICD) Dar es Salaam'






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)