Ukumbi wa Nkurumah uliopo chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.
...........
UGONJWA WA ‘’RED EYES’’ WAANZA KUTIKISA WANAJUMUYIA WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
MIWANI MYEUSI YAVALIWA KUSTIRI MACHO YA WAGONJWA
NANI ALAUMIWE UCHEREWESHWAJI WA PESA ZA KUJIKIMU ZA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
UGUMU WA MAISHA WAENDELEA KUWA GUMZO MITAANI NA MAOFISINI
KUMBE 90% YA WANAFUNZI WA UDSM WANATEGEMEA BOOM KUENDESHA MAISHA YAO
Ikiwa
ni hali ya kawaida ya kila mwaka wakazi wa chuo kikuu cha Dar es salaam
na maeneo jirani kukumbwa na ugonjwa wa macho maarufu kwa jina la RED
EYES, Ugonjwa huo umerudi tena ambako wagonjwa mbalimbali wameripotiwa
kuugua ugonjwa huo. Mlimani leo ilipiga kambi hospitali ya Chuo Kikuu cha
Dar es salaam na kujionea wagonjwa mbalimbali waliojitokeza kupatiwa
tiba hiyo.Hata hivyo wengi wa wagonjwa walionekana wakiwa katika hali ya
awali ya ukuaji wa ugonjwa huo kwani macho yao hayakuonekana kuwa
mekundu sana na macho kuvimba kama ilivyo kawaida ya ugonjwa huo katika
dalili zake.Mlimani leo ilimtafuta Mganga Mkuu wa Hospitali ya chuo hicho
kueleza mwenendo mzima wa ugonjwa huo na pengine idadi ya wagonjwa
waliofika katika hospitali hiyo kupatiwa matibabu ambako ilielezwa
yakwamba alikuwa nje ya ofisi.Nao baadhi ya wagonjwa walioambukizwa na
ugonjwa huo walionekana kuvaa miwani myeusi kusitiri macho yao mbele za
watu.
MLIMANI LEO TUNAPENDA KUWAPA POLE WAGONJWA WOTE WALIOAMBUKIZWA NA
UGONJWA HUO. AIDHA TUNAPENDA KUWASHAURI WAKAZI WOTE WA CHUO KIKUU CHA
DAR ES SALAAM KUZINGATIA USAFI MARA KWA MARA, IKIWA NI PAMOJA NA KUNAWA
KWA SABUNI,KUTOSHIKANA MIKONO NA MGONJWA AU KUSHIKA
VYUMA/MBAO (‘’BALIKONZI’’) ZILIZOPO KANDO YA NGAZI ZILIZOPO KATIKA
HOSTELI ZETU . KUTOKUMBATIANA NA MGOJWA ILI KUWEZA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI
HAYO. PAMOJA NA HAYO JAMBO HILO LIFANYWE KWA NIA NJEMA ISIJE KUONEKANA
YAKUWA TUNAWATENGA WAGONJWA.
Ø NANI ALAUMIWE UCHEREWESHWAJI WA PESA ZA KUJIKIMU ZA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Pamoja
na serikali kujitahidi kutoa fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa Elimu
ya juu hususani Chuo Kikuu cha Dar es salaam mapema kabisa, Zamu hii hali
ilikuwa tafauti kwa utoaji wa huduma hiyo. Hali ilikuwa ngumu kwa wanafunzi hususani
wanaotegemea ‘boom’ ambao wengi wao walikuwa mitaani na wengine wakiwa
wameenda makwao.Hili lilijidhihirisha juma la kwanza wakati chuo
kimefunguliwa ambako hapakuwepo wanafunzi katika viunga vya udsm ingawa
ni vigumu kusema hawakuwepo kabisa.Wanafunzi hawa wawe wa kike au
wakiume wengi wao wanategemea ‘boom’, jambo ambalo liliwawia gumu kutoka
makwao mikoani kwani wanategemea boom kwa mambo mengi,mambo hayo
yanatofautiana baina ya mtu na mtu.Wapo wanao tunza wazazi
wao,wanaojilipia ada wenyewe tena kwa asilimia kubwa, wapo waliokuwa
wanategemea nauli itoke kwenye boom hilohilo,wapo wanaopanga mitaani
ambako wanalazimika kulipa pango la nyumba tena kwa miezi sita,wapo
wanao tunza wadogo zao kwani inawezekana katika familia mwanafunzi huyu
ndiye wa kwanza mwenye uwezo wa aina hiyo.Kwa ujumla hadithi ni nyingi
juu ya matumizi ya pesa hizi kulingana na mtu mwenyewe.Katika juma
hilohilo la kwanza Mlimani leo ilishuhudia mambo kadha wa kadha.Kwanza
hapakuwepo usajili wa wanafunzi na hii si kusema kwamba wahusika wa
kutoa huduma hiyo hawakuwepo bali wakusajiliwa hawakuwepo. Pili ni juu
ya jitihada zilizokuwa zinafanywa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam katika kufuatilia Stahiki za wanafunzi ambako ndugu Prof. Yunusu
Mgaya alitoa taarifa kwa umma zaidi ya mara mbili kuwataka wanafunzi
wawe watulivu,Kiongozi huyo alisema endapo pesa ikifikia hatua ya uwezo
wa kimamlaka Uliyonayo chuo, kitatoa pesa hizo kwa wanafunzi. Tunafikiri
Prof. lilikuwa jukumu lake kufanya hivyo kwa kuujulisha umma lakini pia
inawezekana aling’atwa na nyoka katika semista ya kwanza kwa kushuhudia
vurugu kubwa.Kwa hiyo alikuwa sahihi kumuona mjusi na kushtuka.
Pamoja
na hayo cha kushangaza hata wafanyakazi wa chuo walicheleweshewa pesa
zao kwa kutoingia kwa wakati.Na hili kuweka uwazi Prof. Mgaya
aliambatanisha matangazo hayo mawili kwa pamoja kuonyesha tatizo si tu
kwa wanafunzi bali hata kwa wafanyakazi wa chuo.Alichokuwa na imani
Prof. mgaya ni kuwa wafanyakazi wasinge andamana mpaka utawala au
kuitisha Rv.squre(Hawa wanakufa kimoyomoyo).
Mlimani leo
tunayasema haya kwa nia njema kabisa, na ndipo inakuja hoja ya NANI
ALAUMIWE.Je tumlaumu Rais Kikwete, Waziri wa Elimu Ndugu
Kawambwa,Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ndugu George Nyantega,Makamu Mkuu
wa Chuo ndugu Prof. Mukandara,Ndugu Prof. Mgaya, Afisa Mikopo wa chuo
ndugu Silivanus au Rais wa Daruso ndugu Kilawa Saimoni na Mawaziri wake
husika.Mchawi yuko wapi katika hili?.Upo usemi ati kila mtanzania siku
hizi analalamika, awe kiongozi au si kiongozi.Na sisi tunapenda kwa moyo
mkunjufu kabisa tuwe watanzania wakwanza wanaolalamika kwa hili.
Wafanyakazi
wa chuo kukosa mishahara yao kwa wakati siyo peke yao,wapo pia askari
polisi walicheleweshewa pesa zao,walimu nao walikuwa katika orodha hiyo,
wapo pia mabalozi wanao wakilisha nchi yetu nao walicheleweshewa pesa
yao ingawa hapa Ikulu ilikanusha jambo hili.
Je hapa mchawi ni Prof.
Mgaya au Mh, Rais .Je ni kweli tukisema tuilamu BODI ya Mikopo,hiyo bodi
inahusika kutoa mishara ya wafanyakazi.Je mamlaka ya chuo katika
kufuatilia stahiki za watu wake zinaishia wapi.Kama kweli mishahara na
posho za wanafunzi zinacheleweshwa kwa sababu tuna watumishi wavivu hasa
hapa kwetu ni dhahiri wawajibishwe kwa mujibu wa sheria,Kama tuna
viongozi wa Daruso wanaopendelea kuitwa waheshimiwa bila kufanya kazi
nao hawatufai,Kama pesa zinaingia kwenye akaunti ya chuo zinapangiwa
shughuli nyingine nao pia viongozi wa aina hiyo hawatufai.Kama tunanunua
mashangingi makubwa ya zaidi ya milioni 200, tunaagiza maua na meza za
ofisini nje ya nchi tunategemea nini.Na anayeagiza hapa si Kikwete ni
watumishi wa sekta husika.Makongamano na warsha haziishi.
Mkurugenzi
badala ya kwenda peke yake kwenye semina analazimika kuondoka na
msafara, mwisho wa siku tunafikia hatua ya kukopa Benki ya Standard
charted au Exim Bank ili
tuwalipe mishahara wafanyakazi. Matumizi yanakuwa makubwa mno zaidi ya
kile tunachoingiza.Je sisi na wewe tuko upande gani. Ndugu yetu ambaye
hujaajiriwa umejipangaje na
hili.Je tunachambua mfumo mzima wa utoaji fedha na kuridhika nao,je ni
endelevu na utakomboa vizazi vijavyo. TUNAOMBA KUTOA HOJA!!
Tukutane Toleo Lijalo,Kwetu Pakavu Tutilie Mchuzi.
MHARIRI MKUU 0718732487 E-mail athumanidrisa@rocketmail.com, MHARIRI MKUU MSAIDIZI +255718169191 E-mail anthonlouismwangake@rocketmail.com






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)