Millen
Magese (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo na
wabunifu watakaokwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki
katika maonyesho ya 'South Africa Fashion Week'
WABUNIFUwatatu, Doreen Estazia Noni anayetumia Lebo ya eskado bird,
Jamila Vera Swai na Evelyne Rugemalira wamepata nafasi ya kuchaguliwa
kwenda kwenye maonyesho ya mitindo yajulikanayo kama South Africa
Fashion Week nchini Afrika kusini kupitia kampuni ya Millen Magese Group
company Limited.
Wabunifu hao
watapanda jukwaani siku ya Aprili Mosi katika onyesho linalobeba jina
la Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX) by Millen Magese
introducing Eskado Bird, Jamila Vera Swai and Evelyne Rugemalira. Millen
alipata fursa ya kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa
wabunifu katika fani hiyo na kuhamasika kuwachukua na kushiriki katika
maonyesho hayo maarufu ya mitindo katika bara la Afrika.
Alisema
kuwa amevutiwa sana na jinsi walivyokuwa wabunifu na hivyo kuhamasika
kuwapa nafasi hiyo ya kujitangaza kimataifa kwa mara ya kwanza katika
historia ya Tanzania kupitia mradi huu anbao pia dhumuni lake kutangaza
vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa. Alifafanua kuwa mpango huu pia
una lengo la kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo dunia nzima
kama New York fashion week, London Fashion Week, Lagos Fashion week na
Milan Fashion week.
Alisema
kuwa hayo yanawezekana kutokana na uzoefu wake wa miaka nane katika
fani ya mitindo na mahusiano mazuri kati yake wadau wa mitindo. Mbali ya
wabunifu hao, Millen pia amewapa nafasi wanamitindo watatu, Anastazia
Gura (21) na mapacha, Victoria Casmir (20) na Victor Casmir kuonyesha
mitindo katika maonyesho hayo ya Afrika Kusini.
Wanamitindo
hao wamepata nafasi hiyo baada ya kuwashinda wengine 486 waliofika
katika usaili uliofanyika kwenye hotel ya Serena chini ya majaji,
Mustapha Hassanali, Ritha Poulsen na mwanamitindo maarufu Aminat Ayinde
kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12.
Mbali
ya wanamitindo hao Millen pia ameingia mkataba wa kufanya kazi na
mwanamitindo wa kiume, Benard Chizi ambaye pia alishinda katika usaili
huo na pia ataungana na wenzake kwenda Afrika Kusini. Millen pia
alionyesha kusikitishwa na wanamitindo maarufu ambao walikuwa
wanawasiliana naye akiwa Afrika Kusini kutaka kusaidiwa kufika hatua za
kimataifa. Alisema kuwa cha kushangaza, wanamitindo hao, hawajajitokeza
katika usaili huo na kumsononesha sana.
“Hii
inaonyesha jinsi gani wanamitindo hao hawajiamini, usaili wangu ulikuwa
fursa pekee ya wao kuonyesha vipaji vyao kimataifa, hata hivyo
hawakufika, nawapongeza waliofika kwani wameonyesha kuwa wanania na
ninaamini watafanya vyema huko Afrika Kusini,” alisema.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Tabasamu Pr Consultancy
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)