Rais,
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati akifungua warsha ya siku
mbili ya mikakati ya kiuchumi ya kuondoa umaskini iliyoandaliwa na
REPOA katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam, leo.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akimpongeza Katibu Mtendaji wa Tume ya
Mipango, Dkt. Phillip Mpango kwa mada nzuri. Katikati yao ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther
Mwaikambo, (kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel
Wangwe, na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt. Ad Koekkoek.
Profesa
Do Duc Dinh, kutoka Vietnam akitoa mada ya jinsi nchi yake
ilivyofanikiwa kuondoa umaskini wakati wa warsha ya siku mbili ya
utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini nchini Tanzania.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa
Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek, Katibu
Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt. Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam Mh Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya
White Sands Hotel alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti, leo.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na Profesa Ibrahim Lipumba,
baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti
juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini, nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)