*Atumia siku sita njiani kutoka Dar hadi Ruvuma
MWANAFUNZI
wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala,
mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18),(pichani) aliyepotea
jijini humo Machi 18 mwaka huu, amepatikana Mbinga mkoani Ruvuma.
Kijana huyo aliyekuwa mgeni jijini Dar es Salaam alipotea siku nne tu tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia ya Franco, kijana huyo alifika kwao Mbinga mkoani Ruvuma Machi 23, akiwa peke yake.
Inadaiwa kuwa, baada ya kufika kwao, alisema kuwa hajui alifikaje huko akiwa ametumia takribani siku sita njiani kutoka Dar es Salaam.
Machi 18 asubuhi, Franco aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa anakwenda kwa shangazi yake, Adela Kisongo, Kariakoo jijini humo, na hakufika alikotarajiwa kufika kama alivyoaga na pia hakurudi shule, na haikufahamika alikowenda.
Walimu na walezi wa kijana huyo, walitoa taarifa Polisi, na wakatumia RB namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta.
Wazazi na wanafamilia ya Franco wanawashukuru wote ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki kumtafuta kijana huyo, aksanteni.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)