Mnamo Tarehe 15 Mwezi wa 3 2012 Blogu ya Lukaza iliwahi kupost habari ya Kijana Shabani Issa ya kuomba msaada wa Kwenda kupata Matibabu kutokana na hali yake ya Jicho kuwa na Uvimbe hivi sasa Kijana Shabani Issa anaendelea Vizuri baada ya Kupata matibabu katika Hospitali ya St Benedict Ndanda iliyopo Mkoani Mtwara.Kwa habari ya Kwanza ya Kijana Issa Kuomba Msaada BOFYA HAPA
Kijana Shabani Issa Akiwa katika Hospitali ya St Benedict iliyopo Mkoani Mtwara baada ya kufanyiwa upasuaji.
Shabani Issa afanyiwa upasuaji jana(27/3/2012)
St.Benedict's hospital Ndanda mkoani Mtwara.Anaendelea vizuri mpaka
sasa.Namshukuru yeye aliyesimamisha mbingu bila kuweka nguzo kwa mema
yake yote ktk shida ya kijana huyu.Nawashukuru wadau walioweza kuchangia
kwa namna moja au nyingine.Najua wengine walijua ni uongo natafuta
namna ya kuneemesha tumbo na wao nawashukuru pia.Naishukuru hospital ya
Ndanda hasa dr.Mathew Ng'onye na Z.A Umbaro kwa jitihada zao ktk
kufanikisha upsuaji salama.Mungu awabariki sana
Mtandao Wa Lukaza Blog Unapenda Kutoa shukrani Kwa Wadau Wote Waliowezesha Kijana Huyu Kupatiwa Msaada wa Kupata Matibabu Katika Hospitali ya Mtakatifu Benedict iliyopo Mtwara Mungu Awazidishie pale mlipotoa Kwa Kujali na Kuonyesha Upendo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)