Kutoka
kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Bi.
Gladness Mkamba akionyeshwa malikia katika mzinga wa nyuki wasiouma na
Afisa Nyuki, Bw. Chescho Japhety (aliyeshika bisibisi) huku Mwandishi wa
Habari wa Gazeti la Mtanzania, Bw. Kambi Mbwana akishuhudia tukio hilo
walipotembelea maeneo ya ufugaji nyuki wilayani Manyoni, mwishoni mwa
wiki iliyopita.
Kutoka
kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, Bi.
Gladness Mkamba akiwaelekeza jinsi ya kutoa asali kwenye sega kwa
mwaandishi wa habari wa Gazeti la Mtanzania, Bw. Kambi Mbwana (mwenye
fulana) na Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Bi. Hellen Ngoromera
ikiwa ni sehemu ya ziara iliyolenga kuwajengea uwezo wa kuelimisha jamii
kuhusu shughuli za ufugaji nyuki nchini. Katika Ziara hiyo waandishi
wa vyombo mbalimbali walipata fursa ya kutembelea vikundi vya ufugaji
nyuki katika Wilaya ya Manyoni na Singida mkoani Singida, mwishoni mwa
wiki iliyopita.
HAWA SI MABWANA
NYUKI NI WAANDISHI WA HABARI WAKIWA WAMEVAA VIFAA MAALUM KWAAJILI YA
KURINA ASALI, KUTOKA KUSHOTO NI MWANDISHI WA STAR TV, STEVEN CHEGERE,
MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MTANZANIA, BW. KAMBI MBWANA, MWANISHI
WA CHANNEL 10,BW. KIBWANA DACHI, NA MWANDISHI WA GAZETI LA UHURU, BW.
MOHAMED ISSA WAKIWA TAYARI KWENDA KUJIFUNZA JINSI YA KURINA ASALI
KATIKA ZIARA HIYO.
BAADA YA KAZI NGUMU WAANDISHI WALIJIPOZA NA ASALI Na Tulizo Kilanga
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)