Muhidini
Issa Michuzi akishikiriana na Uhuruone wanawapatia wakazi wote wa Dar
es Salaam huduma ya “Wifi hotspots” ambayo itawapa wakazi wote wa Dar es
Salaam huduma ya bure ya kutembelea tovuti ya Michuzi. Kwa kupitia
mitambo yao ya “Wifi Mesh” iliyopo Dar es Salaam ambayo imeunganishwa na
tovuti ya Michuzi,wakazi wa Dar es Salaam wanatangaziwa kwamba wawashe
kompyuta zao na kuunganishwa na taarifa za punde bila gharama yoyote.
Akikaririwa
katika mahojiano ndugu Issa Michuzi alisema hivi, “Ni mapinduzi ya
kweli ambapo Watanzania wanachukua hatua katika kuleta taarifa
mbalimbali kwa wananchi katika viwango nafuu. Ninaamini hii itaongeza
mawasiliano kwa watu wetu na ni ndoto yangu kwamba tovuti ya Michuzi
itakua huru kufika kwa Watanzania wote hivi karibuni”.
Akiwa
ofisini Bwana Rajabu Katunda alisema, “Uhuruone imejikita katika kutoa
huduma kwa jamii na tumegundua kwamba taarifa za kijamii zinatakiwa
kuwafikia wanajamii kwa urahisi. Tovuti nyingi zinatembelewa na
Watanzania waliopo nchi za nje kuliko wananchi waliopo nchini na hii
siyo haki. Kama nina uwezo kupata taarifa kwenye tovuti ya Michuzi ni
jukumu letu kama kampuni kuwawezesha watanzania waliopo nchini pia
kupata huduma. Watanzania tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kusaidiana na
kupeana moyo na hii itasaidia kukuza uchumi wetu sio tu kununua na kuuza
bidhaa kutoka nje.
Kwa
pamoja Bwana Michuzi na Katunda wamesema huu ni mwanzo tu na wanaamini
kwamba hili wazo litafuatwa na wengine. Kwa msisitizo Bwana Michuzi
aliongea “Lazima tuonyeshe mfano kwa vitendo sio maneno tu. Tumechukua
hatua ya kwanza katika kufanikisha ndoto, wengine wanatakiwa kujiunga
kwenye mapinduzi haya na kufanikisha”
Kutembelea
tovuti ya Michuzi bila gharama washa Wifi kwenye Ipad, Tablet, Simu au
Laptop. Tafuta Michuzi blog Wifi, Unganisha ,fungua browser yako
uipendayo mfano Chrome, Internet Explorer, Safari au Firefox na nenda
kwa Issa Michuzi.blogspot.com.
Kama hautaona tovuti ya Michuzi Wifi, tafadhali wasiliana na Uhuruone kwa email ifuatayo, issa.michuzi@uhuruone.com au piga simu namba 255779477477 ili uweze kuunganishwa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)