Na Joachim Mushi, Kisarawe
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo umepeleka
baadhi ya waandishi wa habari za uchunguzi wilayani Kisarawe, Mkoa wa
Pwani kuangalia matokeo ya utafiti walioufanya mwaka 2010 juu ya baadhi
ya huduma za jamii hasa za afya na maji eneo hilo.
Akizungumza wilayani Kisarawe Ofisa Habari wa TGNP, Kenny Ngomuo
alisema wameamua kupeleka baadhi ya waandishi wa habari kuangalia
mrejesho wa utafiti walioufanya mwanzoni mwa mwaka 2010 kuangalia huduma
mbalimbali za msingi kwa jamii.
Mwaka 2010 TGNP ilipeleka timu ya waandishi wa habari wilayani
Kisarawe kufanya uchunguzi na kuibua kero mbalimbali ambazo zilikuwa
zikiwakabili wakazi wa eneo hilo.
Akitoa taarifa fupi kwa wanahabari na waandishi wa habari na
wanaharakati Bi. Ngomuo alisema waandishi hao watatembelea vijiji
mbalimbali ambavyo vilihusishwa katika uchunguzi wa awali na kuangalia
tofauti iliyopo sasa ikiwa ni miaka takriban mitatu tangu kufanyika kwa
uchunguzi wa awali.
Alisema waandishi hao watafanya mahojiano na wananchi, wanaharakati
na baadhi ya viongozi wa kata zilizofanyiwa utafiti kuangalia tofauti
iliyopo tangu kufanyika kwa uchunguzi wa awali, ikiwa ni pamoja na
kutembelea maeneo ya huduma za jamii katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)