TBL YASAIDIA MAGODORO 200 NA VYANDARUA 200 HOSPITALI YA KILIMANJARO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TBL YASAIDIA MAGODORO 200 NA VYANDARUA 200 HOSPITALI YA KILIMANJARO



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akisoma hotuba ya kushukuru Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa msaada wa mgodoro 200 na vyandarua 200 vyenye thamani ya Sh. mil. 15 katika hafla iliyofanyika mwanzoni mwa wiki, mjini Moshi. Hospitali ya Kilema itapata msaada wa magodoro 100 na vyandarua 100 na Hospitali ya Wilaya ya Hai itapata magodoro 100 na vyandaruwa 100.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (wa tatu kushoto) akikabidhi moja kati ya magodoro 100 na vyandarua 100 kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kilema iliyopo Moshi vijijini, Dk. Wonanji Timoth msaada uliotolewa kwa hospitali hiyo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),katika hafla iliyofanyika mwanzoni mwa wiki.Tbl ilitoa pia msaada kama huo kwa Hospitali ya Wilaya ya Hai. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steven Kilindo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo (kushoto) akimkabidhi godoro Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama ikiwa ni sehemu ya msaada wa magodoro 200 na vyandarua 200 vyenye thamani ya sh. mil. 15 vitakavyogawiwa kwa Hospitali za Kilema na Hai mkoani humo. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Moshi.
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali hiyo, wakishuhudia makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages