MARUDIO
ya kura ya maoni ya kutafuta Mgombea Ubunge wa chama cha Mapinduzi
(CCM) Jimbo la Arumeru Mashariki yaliyofanyika jana, yamemtangaza, Siyoi
Sumari, kuwa mshindi katika mzunguko wa pili wa kura hiyo ya maoni.
Siyoi ameshinda kura hizo za maoni kwa kura 761 dhidi ya mpinzani wake William Sarakikya ambaye alipata kura 361.
Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, iliagiza kurudiwa kwa kura ya
maoni ikihusisha wagombea hao baada yao na wengine waliojitokeza
kutofikisha zaidi ya nusu ya kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la
Arumeru Mashariki.
Katika kura hizo, Siyoi aliongoza kwa kupata kura 361 akifuatiwa na Sarakikya aliyepata kura 259. Kamati Kuu ilifanya uamuzi huo ili kupata mgombea ambaye atapata asilimia 50 au zaidi ya hapo.
Matokeo ya jana yalitangazwa na Msimamizi, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa. Wajumbe waliopiga kura walikuwa 1,124 ambapo kura mbili ziliharibika.

Sumari sasa anasubiri baraka za CC ya chama chake kumpa mikoba ya kutetea kiti hicho kilicho achwa wazi na Marehemu baba yake.
Wakati huo huo habari
kutoka huko Arumeru zinapasha kuwa, Mfanyabiashara maarufu mkoani
Arusha anayechimba, kuuza na kununua madini aina ya Tanzanite, Thomas
Mollel ‘Askofu’ amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa madiwani.
Askofu huyo ambaye ni Diwani wa Mbuguni, Arumeru, alikamatwa usiku wa kuamkia jana kwa tuhuma hizo zinazohusiana na kura ya maoni ambayo ilipigwa jana .
Askofu kukamatwa, ilidaiwa kwamba alikutwa kikaoni akishawishi madiwani kwa rushwa ili wampigie kura ya maoni Siyoi, ili apate ridhaa ya CCM kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.
Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Arusha, Mbengwa Kasomambuto, alidai kwamba hadi jana walishamkamata Askofu na watuhumiwa wengine wawili.
Kasomambuto alidai kuwapo mtandao wa kutoa rushwa na kwamba Askofu alikabidhiwa kazi ya kushawishi kundi la madiwani hao na juzi juzi kukutana na baadhi yao kwenye kikao ambacho hakikuwa rasmi wala halali.
Aliwataja wengine waliokamatwa, kuwa ni Elirehema Kaaya ambaye awali aligombea katika mzunguko wa kwanza wa kura hiyo lakini alishindwa kwa kupata kura 205.
Ilidaiwa kuwa naye alihusika kushawishi waliompigia kura awali, ili wampigie Siyoi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana. Mwingine ni Ezekiel Mollel, ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Vijana ya CCM Wilaya ya Monduli.
“Wote watatu tunawashikilia na wako kwa uchunguzi zaidi na ukikamilika wote watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa,” alisema Kamanda huyo.
Aliongeza kuwa Elirehema ni Katibu Mwenezi wa CCM Nyamagana ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo. Alidai kwamba mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa, alikutwa na tuhuma za kupewa jukumu la kushawishi kwa rushwa wajumbe waliompigia kura katika uchaguzi wa awali wapatao 205 ili wahamishie kura zao kwa Siyoi.
Kuhusu Mollel aliyekamatwa juzi, Kasomambuto alidaiwa kwamba alikutwa Arumeru akishawishi kundi la vijana wampigie kura Siyoi. Alisema Takukuru inaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine zaidi ya watatu waliokimbia kutoka kikao hicho kwenye baa ya Levis katika kata ya Maji ya Chai, Arumeru.
Pia Takukuru inashikilia pikipiki mbili zilizokutwa eneo hilo; moja ikidaiwa kuwa ya Katibu Hamasa wa UVCCM Arumeru, John Nyiti.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)