Kamati
kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM leo imemteua Sioi Sumari kuwa mgombea wa
ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika jimbo la Arumeru Mashariki ,
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jioni hii katika ofisi
ndogo ya CCM Rumumba Katibu mkuu wa CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye
amesema.
"Chama hicho pia
kimemteua Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kufungua kampeni hizo na
kufunga lakini pia jukumu la kampeni liko kwa wanachama wote wa CCM
wakiwepo viongozi walioko eneo husika.
Chama
hicho pia kimemteua Katibu wa CCM Fedha na Uchumi Bw. Lameck Nchemba
Mwigulu kuwa mratibu wa kampeni hizo, Katika hatua nyingine Nape amesema
"Chama kimetoa baraka kwa Tasisi ya Kupambana na rushwa TAKUKURU
kuendelea na mchakato wao wa kushughulikia watu waliokamatwa na rushwa
katika kura za maoni za CCM jimboni humo, na akaipongeza sana TAKUKURU
kwa hatua hiyo.
Uchaguzi wa Jimbo la Arumeru
unafanyika tena baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Jeremiah Sumari
kufariki dunia hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)