AIRTEL yafanya kampeni ya KUENDESHA+SIMU= KIFO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AIRTEL yafanya kampeni ya KUENDESHA+SIMU= KIFO

 Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel,Jane Matinde akionesha aina ya kipeperushi chenye ujumbe wa usalama wa barabarani (stika) ambayo inabandikwa kwenye magari mbalimbali.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki akishirikiana na viongozi wa usalama barabarani akibandika  machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary ya Dar es Salaam kulia ni kamanda Jeshi  la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga, kushoto ni  Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde  akishuhudia zoezi  hilo.
Kamanda  Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga, akibandika   machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na  club ya Rotary  yenye ujumbe wa kuendesha +simu =kifo  kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi, ulia ni  ni Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia zoezi hilo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki (wa tatu kutoka kulia  mwenye miwani)  akishirikiana na viongozi wa Usalama barabarani pamoja na viongozi wa Club ya Rotary ya Dar es Salaam kubandika machapisho ya Usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuhakikisha kuwa  madereva wanaendesha kwa usalama zaidi bila kutumia siku za mkononi. Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mh. Mohamed Mpinga, muwakilishi kutoka Club ya Rotary Dar es Salaam, Bw. Zainul Dossa pamoja na Bw. Hamza kassongo. 

Serikali  imesema kutokuwepo kwa sheria ya barabarani inayozuia matumizi ya simu za mkononi wakati wa uendeshaji wa  vyombo vya moto kunachangia kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria madereva ambao waonekana kutumia simu za mkononi huku wakiwa wanaend zesha vyombo
hivyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis kagasheki wakati wa zoezi la kubandika ujumbe katika magari mbalimbali  unaokataza matumizi ya simu za mkononi wakati wa kuendesha vyombo vya moto. Ni kweli hadi sasa hakuna sheria inayomkataza moja kwa moja dereva
kuacha kutumia simu awapo barabarani lakini naomba wananchi wafahamu kuwa hili linafanyiwa kazi na wafuate maelekezo yalioyotolewa na wadau kama hawa ambayo kiukweli yanatoa elimu ya kupunguza madhara ya ajali za mara kwa mara” alisema Balozi Khagasheki.

kwa mujibu wa tathmini ya jeshi la polisi baadhi ya ajali  nyingi zinazotokea barabarani zinatokana na matumizi ya smu za mkononi wakati  wa kuendesha vyombo vya moto hali inayopelekea kuongezeka kwa ajali nyingi na kusababisha vifo  ambavo  vingeweza kuzuilika kwa urahisi. Balozi kagasheki amesema kuwa upungufu wa kutokuwa na sheria ya kuzuia matumizi ya simu za mkononi wakati  kuendesha gari unapelekea kushindwa kuwachukulia hatua kali madereva ambao wanaonekana kufanya hivyo.

Naye muandaaji wa zoezi hilo Zeinul Dossa kutoka klabu ya Rotary ya jijini dare s salaam pamoja na Jene matinde afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wamesema kuwa zoezi hilo la kubandika ujumbe huo litafikisha ujumbe kwa madereva wengi  pamoja na kupunguza ajali. Zaidi ya machapisho elfu 5 yametengenezwa kwa ajali ya kubandika pamoja na kusambazwa katika magari mbalimbali  ambayo yatarahisisha kupunguza ajali za barabarani ambazo zinaweza kuzuilika kwa kshirikiana na jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages