Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ameagiza Kusitishwa Mara Moja Kwa Shughuli Zozote za Ujenzi wa Maradi wa Hoteli Katika eneo la Nungwi Mashariki lenye Lenye Ukubwa Wa Hekta 30.5. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ameagiza Kusitishwa Mara Moja Kwa Shughuli Zozote za Ujenzi wa Maradi wa Hoteli Katika eneo la Nungwi Mashariki lenye Lenye Ukubwa Wa Hekta 30.5.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Akimpatia mkopo Bibi Mwamvua Juma Hussein kutoka katika chama cha akiba na mikopo cha Mkwajuni mara baada ya kuzindua Afisi yao
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa Skuli ya Kidagoni kusoma kwa bidii mara baada ya kuweka jiwe la msingi la skuli yao mpya inayojengwa kwa nguvu za Wazazi wao.
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Kidagoni katika Jimbo la Nungwi ambao hivi karibuni wanatarajiwa kuondokana na mazingira mabovu ya eneo la kusomea la banda la makuti baada ya jingo lao jipya likiwa katika hatua za mwisho kukamilika.
----
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameagiza kusitishwa mara moja kwa shughuli zozote za ujenzi wa Maradi wa Hoteli katika eneo la Nungwi Mashariki lenye ambalo linaukubwa wa Hekta 30.5.

Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara yake ya siku tatu ya kutembelea Miradi ya Maendeleo na ile ya Kijamii ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja .

Balosi Seif alisema zipo dalili za ujanja zinazoonekana kufanywa na Maafisa wachache na kupelekea mgongano na malalamiko ya umiliki wa eneo hilo kufuatia kufuta kwa mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Kitalii wa Kampuni ya Spice Island kwa madai ya kukiuka masharti.
Balozi Seif alikemea tabia inayofanya na baadhi ya Watendaji wa Idara ya Ardhi ambayo inawabughudhi Wawekezaji na hatimae kuitia aibu Serikali.


“ Inashangaza kuona Idara ya Ardhi inamfutia mkataba muekezaji mmoja kwa kushindwa kutekelezaa mkataba ndani ya miaka miwili, lakini idara hiyo hiyo kumpa mwekezji mwengine kwa zaidi ya miaka saba bila ya kumvunjia ”. Balozi Seif alisema lipo jambo katika mradi huo.

“ Kuanzia sasa nasema sitaki kuona shuguli yoyote ya ujenzi inaendeshwa katika eneo hili hadi Serikali Kuu itakapofanya maamuzi baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusiana na mgongano huo”. Balozi Seif alikuwa akimuagiza Afisa wa Ardhi Bwana Sanani Baraka kufanya kutekeleza agizo hilo.

Kwa upande waoWananchi wa Kijiji cha Nungwi wameelezea masikitiko yao kutokana na mgongano huo unaopelekea kucheleweshewa maendeleo yao ya Kijamii kupitia makubaliano ya Mradi wa mwanzo ambao tayari ulikuwa umeshakubalika baina yao na mwekezaji wa awali.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliweka jiwe la msingi la Afisi ya Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Mkwajuni na kuwapongeza kwa uamuzi wa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 ya kuendeleza Vikundi vya Ushirika.
Balozi Seif alisema Wanachama hao bado wanahitaji kukuza Chama chao ili kukijengea mazingira mazuri ya kujipatia mahitaji yao.

Baadaye Balozi Seif aliweka jiwe la msingi la Jengo jipya la Skuli ya Kidagoni iliyoko ndani ya Jimbo La Nungwi.Ujenzi wa Skuli hiyo umekuja kufuatia Watoto wa Vijiji vya Kidagoni na Mwanguo kufuata Elimu katika masafa marefu.

Balozi Seif alisema nia nzuri ya Wazee wa Vijiji hivyo ni hatua ya msingi ya kuwajengea hatma njema ya Kielimu Watoto wao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amewaomba Wananchi hao kuwa na subra kutokana na changa moto wanaopambana nazo za bara bara, maji safi na Kituo cha Afya na kusema Serikali inaangalia njia za kuyatatua matatizo hayo.

Imetolewa Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages