SERIKALI YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA HUDUMA ZA MACHO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SERIKALI YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA HUDUMA ZA MACHO

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akifurahia jambo na mwimbaji na mpiga gitaa mahili wa Bendi ya watu wenye ulemavu (Blind Beat Band) mzee Bonifasi Kiyenze leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini. Bandi hiyo ni miongoni mwa vikundi vya burudani vilivyoalikwa kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Vijana kutoka kikundi cha sarakasi cha Bandi ya Mjomba kikionyesha umahiri katika mitindo mbalimbali ya sarakasi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini.

Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akizindua Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam ambapo Tanzania imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya Glaukoma duniani ambayo imeongozwa na kauli mbiu isemayo “Usiachie Glaukoma isababishe giza kwenye maisha Yako”
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi nakala ya Mpango mkakati wa taifa wa huduma za macho nchini mwakilishi wa waandishi wa habari waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa mkakati huo Bi. Zaina Jongo Malongo kutoka Gazeti la Mwananchi leo jijini Dar es salaam kufuatia umuhimu wa waandishi wa habari katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu sera mbalimbali.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages