GAVANA WA BENKI KUU TANZANIA PROF BENO NDULU NA UJUMBE WA IFM NCHINI WAZUNGUMZA NA WANAHABARI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

GAVANA WA BENKI KUU TANZANIA PROF BENO NDULU NA UJUMBE WA IFM NCHINI WAZUNGUMZA NA WANAHABARI

Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum (kushoto) kumaliza kuongea na waandishi wa habari kuhusu uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
Baadhi ya wajumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi msaidizi wa shirika hilo Peter Allum wakati akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishwa na ukame mwaka 2011. Ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera. (Picha na Anna Nkinda - Maelezo)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages