Naibu
Waziri wa Biashara wa China Li Jinzao (aliyesimama ) akitoa hotuba
jana jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na
misaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya
kuisaidia Tanzania. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri wa Fedha Mustafa
Mkulo (hayupo pichani)kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa
Biashara wa China Li Jinzao. Kulia ni Balozi wa China nchini Lu Youqing.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo(aliyesimama ) akitoa hotuba jana jijini Dar es
salaam wakati wa sherehe fupi ya kusaini mkopo na misaada kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Sherehe hizo zilisainiwa na Waziri
Mkulo kwa niaba ya Tanzania na Naibu Waziri wa Biashara wa China Li
Jinzao (hayupo pichani) . Msaada na Mkopo huo unazidi bilioni 80 Fedha
za Kitanzania. Kushoto ni Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu na kulia ni
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) na Naibu Waziri wa Biashara wa China
Li Jinzao (kulia) wakisaini makubaliano leo jijini Dar es salaam ya
Serikali ya China kuipa mkopo nafuu na msaada kwa ajili ya shughuli
mbalimbali za maendeleo nchini. Msaada na mikopo hiyo ni zaidi bilioni
80 fedha za Kitanzania ambayo inazidi kuimarisha urafiki na undugu kati
ya Tanzania na China.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri
wa Biashara wa China Li Jinzao (kulia) leo jijini Dar es salaam
wakati kiongozi huyo alipokwenda Wizara ya Fedha kwa ajili ya kusaini
mkataba wa mkopo nafuu na msaada wa zaidi ya bilioni 80 za Kitanzania
kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)