Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua Jengo la
Ofisi ya Elimu Wilaya ya Kusini liliopo Makunduchi likikaribia hatua ya
uwezekaji ambapo aliahidi kuchangia Matofali 3000 na Mifuko ya Saruji
30 kukamilishia ujenzi huo.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Abdulla Mzee
Abdulla akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya
Wilaya ya Kusini iliyopo Paje Mtule. Balozi Seif aliagiza kufutwa mara
moja kwa mkataba wa ujenzi na kampuni ya Electric International endapo
hatokamilisha ifikapo mwishoni mwa mwezi wa julai mwaka huu
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliangalia Darasa la
Kompyuta la Charity School iliyopo Bwejuu baada ya kuweka jiwe la
Msingi la Skuli hiyo.Kulia ya Balozi ni Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Mh.
Mohd Ibrahim, Naibu Waziri wa Elimu Mh. Zahara Hamad pamoja na Baadhi
ya Waalimu wa Skuli hiyo ya Maandalizi na Msingi.
--
Kampuni
ya Ujenzi ya Electric International Company Limited imeagizwa
kukamilisha ujenzi wa Skuli Mpya ya Sekondari ya Wilaya ya Kusini
iliyopo Paje Mtule ndani ya kipindi cha miezi minne vyenginevyo
itafukuzwa na italazimika kulipa gharama zote zitakazojiri kuitia
hasara serikali.
Agizo
hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi wakati alipoikagua Skuli hiyo akiwa katika ziara ya Siku moja
ndani ya Wilaya ya Kusini kuangalia Shughuli za Maendeleo na Miradi ya
Jamii.
Balozi
Seif alimuagiza Msimamizi wa Ujenzi huo kwamba Mwishoni mwa Mwezi wa
Julai mwaka huu ahakikishe ahadi aliyoitoa anaitekeleza kinyume na
hivyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali italazimika kuifutia mara
moja Mkataba wa Ujenzi Kampuni hiyo.
Alisema
kitendo cha Makandarasi wa Ujenzi huo kumuahidi rais wa Zanzibar
kwamba watakamilisha kwa wakati uliopangwa ujenzi wa Skuli hiyo
kimeitia aibu Serikali.
“
Inasikitisha kuona Kiongozi Mkuu wa Kampuni hiyo ya Electric
International Company Limited yumo katika Bodi ya Wakandarasi Tanzania.
Si dhani kuwa utumbo kama huu tunaweza kuuvumilia” Alikemea Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar.
Balozi
Seif aliiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
kuhakikisha kwamba Mkandarasi huyo anakabidhi jengo hilo katika muda
alioahidi.
Alisema
kumalizika kwa Skuli hiyo kutasaidia kuondosha upungufu wa Skuli za
Sekondari Wilayani ambao wengi wa Wanafunzi wake hulazimika kufuata
Elimu ya juu sehemu za Mijini.
Mapema
Naibu Katibu Mkuu wa Wiara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Abdulla
Mzee Abdulla alimueleza Balozi Seif kwamba Ujenzi wa Skuli hiyo ya
Baje Mtule umeanza mapema mwaka 2006 kuliko Skuli nyengine zilizomo
ndani ya Mradi huo ambazo tayari hivi sasa zimeshakamilika ujenzi
wake.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika ziara hiyo
aliweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Jamii ya Bwejuu {Charity School }
ambayo imejengwa kwa nguvu za wahisani na Wananchi wenyewe.
Akizungumza
na Walimu, Wazazi, Kamati ya Skuli na Wanafunzi wa Skuli hiyo wapatao
264 wa Maandalizi na Msingi Balozi Seif aliwapongeza Wazazi kwa uamuzi
wao wa kuwatengenezea hatma njema ya Elimu Watoto wao.
Alisema
Mkoa wa Kusini Unguja umekuwa na Historia ya kutoa Wataalamu wengi
Nchini kufuatia misingi imara uliopo kwa kipindi kirefu ya kujenga
mazingira bora ya upatikanaji wa Elimu.
Balozi
Seif alihamasika na kuahidi kuchangia Shilingi 1,000,000/- kusaidia
uendelezaji wa Skuli hiyo iliyogharimu zaidi ya Shilingi Milioni Mia
Tisa Nukta Tisa { 994,000,000/- }.
Akilitembelea
Jengo la Ofisi ya Elimu liliopo Makundichi Wilaya ya Kusini Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wa Watendaji hao wa Elimu
Wilayani humo kujijengea Makazi ya kisasa unafaa kupongezwa na kuungwa
mkono.
Balozi
Seif katika kuunga mkono jitihada hizo ameahidi kuchangia Matofali
3,000 na Saruji Mifuko 30 ili kusaidia kukamilisha ujenzi wa Jengo hilo
ili kukabidhiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa hatua za
uwezekaji.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)