Visima vya Maji
Mkazi
wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma Bw.Samwel Chindombwe
akisalimiana na Mkuu wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom
Tanzania(Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule,baada ya kukabidhi
msaada wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 40 katika
kijiji hicho.
Mkuu
wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation)
Yessaya Mwakifulefule,akimtwisha Amina John ndoo ya maji ya kunywa
yaliyochotwa katika kisima kilichotolewa msaada na Vodacom Foundation
kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma,Mradi huo
umegharimu thamani ya shilingi milioni 40.
Mkuu
wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation)
Yessaya Mwakifulefule.(kulia )akiwa na wakazi wa kijiji cha Inyumbu
Mkoani Dodoma wakinywa maji salama yaliyotokana na mradi wa Kisima
kilichojengwa na Vodacom ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi huo wenye
thamani ya shilingi milioni 40 uliotolewa na Vodacom Foundation.
Wakichota maji kwenye bomba mara baada ya mradi huo wa maji kuzinduliwa rasmi
Baadhi
ya wakazi kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma waliohudhuria sherehe ya
uzinduzi wa kisima cha maji salama uliojengwa na V odacom Foundation
Wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma wakicheza wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa visima vya maji.
---
Dodoma: 27.03.12:
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa
kusaidia Jamii (Vodacom Foundation) imekabidhi mradi wa maji wenye
thamani ya shilingi milioni 40 katika kijiji cha Inyumbu ikiwa ni
mwendelezo wa azma yake ya kusaidia jamii hapa nchini.
Kukabidhiwa
kwa mradi huo kunapunguza shida ya upatikanaji wa huduma ya maji safi
na salama kwa wakazi zaidi ya 4,000 wa kijiji cha Inyumbu na maeneo
jirani.
Akipokea
mradi huo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Yona Ngobito aliishukuru
kampuni ya Vodacom kwa kuwekeza shilingi Milioni 40 ili kuokoa maisha
ya wananchi ikifahamika wazi kuwa maji ni bidhaa muhimu na nyeti katika
maisha ya binadamu.
“Kila
msaada ni muhimu kwa walengwa husika ila tunapozungumzia maji tunagusa
moja kwa moja uhai wa binadamu, hili ni jambo jema kwenu wanakijiji wa
Inyumbu ambao sasa wanawake na wasichana wanaweza kutumia muda mfupi
kupata bidhaa hiyo na kutumia muda wa ziada kufanya shughuli nyengine za
kifamilia”Alisema Mwenyekiti huyo.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo wa kijiji ametumia pia fursa hiyo kuwasihi
wanakijiji kuona thamani ya mradi huo na njia pekee ya kurudisha
shukrani kwa Vodacom ni kuutunza mradi huo ili uwasidie kwa muda mrefu
zaidi.
“Ndugu
zangu hasa wakina mama tukitambua shida ambayo tulikuwa nayo hapo
kabla ya kuletewa mradi huu na Vodacom ni wazi tutaona thamani yake na
kila mmoja atakuwa mlinzi wa mradi huu dhidi ya aina yoyote ya
uharibifu, hiyo si tu kwamba itatusaidia kuwa na uhakika wa maji bali
tutawapa nguvu Vodacom kurudi tena kuangalia eneo jingine la
kutusaidia”Aliongeza Ngobito
Nae
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,alisema
Vodacom Foundation imekua ikithamini maisha ya watanzania wengi na hivyo
kujitolea katika kusaidia na kufadhili shughuli mbalimbali za maendeleo
ya kijamii hapa nchini.
Aliongeza
kuwa kutokana na kwamba Mkoa wa Dodoma una ukame katika baadhi ya
maeneo yake na hivyo kuleta changamoto katika upatikanaji wa maji safi
na salama kwamatumizi ya binadamu hasa maeneo ya vijijini jambo
lililoigusa kampuni ya Vodacom kupitia mfuko huo na kufikia uamuzi wa
kufadhili mradi huo wa maji kupitia teknolojia ya upepo.
“Katika
jitihada zetu za kuboresha ustawi wa jamii za watanzania kwa kuwa
washirika wa huduma za kijamii nchini zimetufikisha hapa katika kijiji
cha Inyumbu kukabidhi mradi huu, ni matumaini yangu kwamba sasa mama
zangu wa hapa kijijini wamefurahi kwa kupunguziwa hali iliyokwepo hapo
awali ya kutumia muda mrefu kusaka maji kwa shughuli mbalimbali za
kifamilia”Alisema Mwakifulefule.
Kila
mwaka tunatenga fedha kusaidia maeneo mbalimbali ya kijamii hasa
elimu,afya, maji,mazingira na ujasiriamali, tunafanya hivyi tukitambua
kuwa biashara kwetu ni sehemu moja ila namna tunavyokuwa karibu
kusaidia wale wanaotuzunguka katika baishara zetu ni jambo moja muhimu
sana katika shughuli zetu, tutaendelea kufanya hivyo tukiamini kwamba
azma yetu ya kubadili maisha ya wananchi inatekelezeka”Aliongeza
Mwakifulefule.
Vodacom
kupitia Vodacom Foundation iliufandhili mradi huo kwa shilingi Milioni
40 kupitia Mamlaka ya maji ya kijiji cha Inyumbu kwa kushirikiana na
mradi wa maji wa C.P.P.S,
-Mwisho-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)