Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akifungua mkutano wa jumuiya ya
serikali za mitaa ya Mkoa wa Ruvuma (ALAT) mjini songea jana,kushoto ni
mwenyekiti wa jumuiya hiyo,Bw. Oddo Mwisho ambaye pia ni mwenyekiti wa
halmshauri ya wilaya ya Mbinga.
Mwenyekiti
wa jumuiya ya serikali za mitaa (ALAT) Mkoa wa Ruvuma,Bw. Oddo Mwisho
akizungumza wakati wa mkutano wa jumuiya hiyo jana mjini songea,wa pili
kushoto aliyekaa ni Mkuuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu na kulia
ni Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo,Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Mwandishi
wa habari mkoani Ruvuma ambaye pia ni diwani wa kata ya Namtumbo mkoani
humo,Alpius Mchucha akizungumza wakati wa mafunzo ya kuandika habari za
uchunguzi kwa waandishi 18 wa mkoa huo juzi.
-
Mkuu
wa Operasheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini,Kamishina Paul
Chagonja akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma
juzi,baada ya kutokea vurugu na mauaji ya watu wawili waliopigwa risasi
na polisi walipokuwa wakijaribu kutawanya maandamano ya madereva
pikipiki mjini songea,kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa
Ruvuma,Kamishina Msaidizi Mwandamizi Michael Kamuhanda.
Wajumbe
wa jumuiya ya serikali za mitaa (ALAT) wa mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza
mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu (hayupo pichani) jana mjini songea
wakati wa mkutano wa jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa
halmashauri ya wilaya songea vijijini
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)