Bondia
mahiri wa mchezo wa Kick Boxer, aliyepata kujizolea sifa lukuki katika
mchezo huo kwa kuwasambaratiza wanadada wenzake kadhaa katika mchezo
huo, Pendo Njau, Baada ya kuwa nje ya Ulingo kwa kipindi cha misiku
chache zilizopita amepata mtoto baada ya kuwa nje ya ulingo kwa kipindi
cha miezi kadhaa kutokana na kuwa mjamzito, hivi sasa anatarajia kurudi
ulingoni kwa kishindo baada ya kujifungua salama.
Akizungumza na Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com,
Pendo alisema kuwa hatua aliyoifikia yeye kwa hivi sasa ya kuwa na
mtoto ni hatua muhimu ambayo kila binadamu aliyekamilika hupaswa
kuifikia.
Aidha
Pendo alishindwa kuweka bayana kuhusiana na baba wa mtoto wake na kudai
kuwa muda utakapofika basi atafunguka zaidi na kuweka mambo hadharani.
Akielezea mikakati yake ya sasa atakaporeje upya, Pendo alisema kuwa
tayari amekwishaanza mazoezi madogomadogo ya kujiweka fiti, na baada ya
kuwa fiti atakuwa tayari kupambana na Bindia yeyote atakayejitokeza
kuomba kucheza naye.Habari na Sufiani Mafoto
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)