Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Makamu wa Pili wa
Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Wapanda Mapiki Piki wa CCM hapo ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa uliopo
Amani Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Mjini
ambae pia ni Mbunge Viti Maalum Mh. Tauhida Gallos Nyimbo na Kulia ya
Balozi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf.
--
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi amewataka Wanachama wa Umoja wa Wapanda Mapiki
Piki wa CCM kufanya maamuzi Magumu lakini ya Busara katika kuhakikisha
wanachagua Viongozi bora kwa ajili ya kujenga safu ya Ushindi wa chama
hicho kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Ametoa
wito huo katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliokutana kufanya Uchaguzi
wa Viongozi wake watakaoongoza Umoja huo katika kipindi cha Miaka mitano
ijayo hapo katika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar.
Balozi
Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema CCM
iliwahi kupata uvamizi ndani ya Jumuiya na Baadhi ya Taasisi zake na
hatimaye kupelekea Matatizo hasa katika chaguzi zilizopita.
Alitahadharisha
kwamba wakati umefika kwa Wanachama wa Chama hicho kuwa makini na watu
kama hao hasa katika kipindi hichi kinachoingia cha chaguzi mbali mbali
za Viongozi wa Chama hicho.
“
CCM haioni shida kupoteza wanachama watatu, watano ambao wana tabia na
njama za kukidhoofisha Chama kwa maslahi yao binafsi”. Alisema Balozi
Seif.
Balozi
Seif amewaomba Vijana hao kujisaidia katika kuachana na mifarakano kwa
lengo la kutengeneza safu nzuri ya muelekeo bora wa Uongozi makini.
Akiwapongeza Vijana hao Balozi Seif aliwaomba kuendelea kukiimarisha Chama chao kwani wao ndio nguvu ya Chama wakati wote.
Balozi
Seif ameahidi kwamba kwa kushirikiana na mlezi wa Umoja huo ataangalia
hatua za namna ya kuisaidia Taasisi hiyo muhimu kwa CCM katika masuala
ya uhamasishaji Wanachama.
Katika
Taarifa yao iliyosomwa na Katibu wa Umoja huo wa wapanda Mapiki Piki
Mkoa Mjini Magharibi Nd. Amour Ali Mwinyi amesema Umoja huo umepata
mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake.
Hata
hivyo Nd. Amour alisema Taasisi yao bado inakabiliwa na baadhi ya
changamoto zinazokwaza utendaji wao ikiwa ni pamoja na msingi wa kianzio
cha kuelekea katika uzalishaji mali.
Mapema
Mlezi wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki Mama Asha Suleiman Iddi
amempongeza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni kwa jitihada
zake za kuunga mkono umoja huo.
Mama
Asha ameziasa Taasisi za CCM zinazoingia kwenye uchaguzi kuwachagua
Viongozi wao kwa kigezo cha Uwezo na kuachana na tabia ya kuangalia
udugu au rafiki.
Alisema
tabia hiyo ikiendekezwa inaweza kukijengea mazingira mabovu Chama
katika utekelezaji wa Sera na Majukumu iliyojipangia ndani ya Ilani
yake.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)