
Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Abdillah Jihad Hassan akitoa
hotuba katika uzinduzi wa Bodi ya Z.B.C huko katika Ukumbi wa ZBC Radio
Rahaleo Zanzibar.Kulia kwake ni katibu Wizara hio Ali Mwinyikai na
Kushoto yake ni Mwenyekiti wa Bodi ya ZBC Tatu Ali,

Waalikwa
mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Bodi ya Z.B.C Wakimsikiliza
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na michezo Abdillah Jihad Hassan
hayupo Pichani akitoa hotuba na kuizindua rasmi Bodi hio.Picha na Yussuf
Simai Ali-Maelezo-Zanzibar
--
Na Faki Mjaka-Maelezo
Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Abdillahi Jihad Hassan
amewataka Wajumbe wa Bodi ya Utangazaji ya Shirika la Habari Zanzibar
(ZBC)kuwa makini katika kuendesha Shirika hilo ili liweze kuleta maslahi
kwa Taifa.
Jihad ameyasema hayo leo alipokuwa akizindua Bodi hiyo inayoundwa na Wajumbe saba katika ukumbi wa ZBC Radio Raha leo Mjini Zanzibar.
Amesema
Jamii ya wazanzibari imejawa na matumaini makubwa na Bodi hiyo ambayo
ndiyo mdomo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivyo ubinafsi katika
Chombo hicho ni jambo ambalo linapaswa kuepukwa
Amesema
jukumu kubwa la Bodi hiyo ya Utangazaji Zanzibar ni kuchochea maendeleo
na kuielimisha jamii ambayo imejawa na hamu kubwa ya kutaka kujionea
utendaji kazi wa Bodi hiyoAidha amefahamisha kuwa ili malengo
waliyojiwekea yaweze kupatikana Wajumbe wa Bodi hiyo wanapaswa kufanya
kazi kwa mashirikiano na kuwajibika ipasavyo katika majukumu
waliyopangiwa kwa mujibu wa taratibu.
Ameongeza kuwa patakapokuwa na mashirikiano na uwajibikaji ni wazi jamii itabadilika jambo ambalo litapelekea pia Bodi hiyo kuweza kuheshimiwa na kufanya kazi kwa urahisi
Nao wajumbe wa Bodi hiyo wamemuahidi Waziri huyo kuzifanyia kazi nasaha zake alizozitoa na kuahidi ufanisi katika kazi zao ili kuliletea Taifa maendeleo.
Bodi ya Utangazaji ya Shirika la Habari Zanzibar (ZBC) inaundwa na Wajumbe saba ambao ni Hassan Mitawi,Ahmed Makame,Yussuf Chunda,Hamida Ahmed Mohammed,Hassan Mzee,Ahmed Chwaya ambapo Mwenyekiti wake ni Tatu Ali.
Imetolewa na
Maelezo Zanzibar
Maelezo Zanzibar





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)