Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) yatoa msaada kwa (SHIMBATA) - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) yatoa msaada kwa (SHIMBATA)

Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania(SHIMBATA) Anna Senkoro (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kupokea msaada shilingi milioni 3 na kapeti kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa bao nchini. Wengine ni Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania(SHIMBATA) Monday Likwepa(kushoto) na Afisa Mawasiliano wa TPA Cecilia Korassa(kulia)
Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania(SHIMBATA) Monday Likwepa(kushoto) akipokea mfano wa hundi ya malipo (cheque) kutoka kwa Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Cecilia Korassa(wa pili kulia) leo jijini Dar es salaam ikiwa ni msaada ulitolewa na TPA kwa Shirikisho hilo kwa ajili ya kuendeleza bao nchini . Wengine ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania(SHIMBATA) Anna Senkoro ( wa pili kushoto) na Mjumbe wa SHIMBATA Seleman Juma Salamba(kulia)
Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania(SHIMBATA) Monday Likwepa(kushoto)na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania(SHIMBATA) Anna Senkoro ( wa pili kushoto) wakipokea kapeti kutoka kwa Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Cecilia Korassa(wa pili kulia) leo jijini Dar es salaam ikiwa ni msaada ulitolewa na TPA kwa Shirikisho hilo kwa ajili ya kuendeleza bao nchini na kutumika kama viwanja vya mashindano ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika katikati ya Mwezi Oktoba mwaka huu hapa nchini . Wengine ni Mjumbe wa SHIMBATA Seleman Juma Salamba(kulia)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages