Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akitowa nasaha zake
kwa Wanawake Wanavikundi wa Jimbo la Malindi wakati walipofika kutowa
vifaa vya kujiendeleza vilivyotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Shein na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Balozi Seif,
makabidhiano hayo yamefanyika katika Tawi la CCM Malindi.
Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Iddi,
akitowa nasaha zake kwa Wanawake wa Vikundi vya jimbo la Mtoni katika
tawi la CCM Mtoni, na kuwataka wasiwe wakiwa kwa kutokuwa na mbunge na
mwakilishi wa CCM katika jimbo hilo kwani wao ndio walezi wao mna wako
tayari kutowa msaada wakati wowote wakiwa na shinda katika vikundi
vyao.
Katibu
wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge Zufura Mgeni Mwalim akisoma majina ya
Wanavikundi ili kukabidhiwa vifaa vyao kwa ajili ya kuzalisha mali
katika vikundi hivyo ili kujiegezea kipato katika kazi za amali.
Mwenyekiti
wa UWT Jimbo la Mji Mkongwe Fatma Hamza akitowa neno la shukrani kwa
msaada waliopata kwa vikundi vya jimbo lao baada ya makabidhiano hayo
yaliofanyika tawi la CCM Malindi.
Khadija
Seif akisoma risala kwa niaba ya Wanawake wa Jimbo la Malindi wakati wa
hafla ya kukabidhiwa vitendea kazi kwa vikundi vya Wanawake wa Jimbo
hilo zilizofanyika katika tawi la CCM Malindi.
Wanawake
wa Viongozi wakisikiliza Makamu wa Pili wa Rais akitowa nasaha zake kwa
Wanavikundi wa Mji mkongwe baada ya kukabidhi vitendea kazi vya vikundi
hivyo, vilivyotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Shein na Mke wa
Makamu wa Pili Mama Asha Balozi Seif kwa vikundi hivyo kujiendeleza
kiuchumi na kujiogezea kipato chao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)