
Wananchi
wa wilaya ya Masasi wakipita mbele ya mgeni rasmi wakiwa na mabango
mbalimbali yenye ujumbe tofauti zenye kuelimisha jamii jinsi ya kuzuia
maambukizi ya kifua kikuu.Takwimu zinaonyesha kuwa wagonjwa wa kifua
kikuu wameongezeka zaidi ya mara 5 kutoka wagonjwa 11,753 mwaka 1983
hadi wagonjwa 63,453 mwaka 2010.

Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akipokea maandamano
(Hayapo pichani) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kifua kikuu
duniani yaliyofanyika Kitaifa wilayani Masasi.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara Kanali Mstaafu Christopher Simbakalia na kulia ni Mbunge wa
jimbo hilo Mhe. Mariam Kasembe.

Wananchi wakipita mbele ya mgeni rasmi.

Waendesha
pikipiki wa mji wa Masasi hawakuwa nyuma, wananchi wengi waliziomba
wizara zingine ziige mfano wa Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii
kupeleka maadhimisho ya Kitaifa kwenye wilaya zilizo pembezoni mwa
nchi.

Waendesha
bajaji nao hawakuwa nyuma ambapo walipakia waandamaji katika
kusheherekea maadhimisho hayo.Takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii zinaonyesha vifo vitokanavyo na kifua kikuu vinapungua
ukilinganisha na vifo 4,500 kwa mwaka 2008 hadi kufikia 3,976 kwa mwaka
2009.Picha na Catherine Sungura-Wizara Ya Afya





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)