Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tuzo za waandishi wa habari (EJAT) itakayofanyika hivi karibuni, pamoja na waandishi wa habari wakati akishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kufuatia msaada wa shilingi milioni 10.925.000 ilioutoa kwa baraza hilo kwa ajili ya maandalizi ya tuzo hizo, katika mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya baraza hilo Mwenge jijini Dar es salaam, katika picha katikati ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) na kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda.
Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti
(SBL) akifafanua jambo katika mkutano huo kuhusiana na udhamini wao
katika tuzo hizo, kulia ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Absalom
Kibanda, ambalo limesaidia sana MCT kupata udhamini huo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 10.925.000 kwa Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT) , fedha ambazo Kampuni ya (SBL) imetoa kwa Baraza la Habari (MCT) kwa ajili ya kufanikisha tuzo hizo, katikati ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti.
Kutoka kulia ni Imani Lwinga Meneja wa Habari na mawasiliano kampuni ya bia ya Serengeti,
Absalom Kibanda Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Teddy Mapunda
Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL), Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji (MCT)
na Nandi Mwiyombela Meneja wa Mahusiano ya Umma wa (SBL), wakionyesha mfano wa hundi hiyo kwa wajumbe wa kamati ya maandalizi na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)