Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)Teddy Mapunda kulia
akisalimiana na Galus Lugenge Diwani wa kata ya Mwangata Frelimo,
wakati alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Iringa mjini kwa ajili ya
ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa uvunaji maji hospitalini hapo, anayefuatia
ni Nandi Mwiyombela Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji (SBL),
Caroli Lunyili Injinia wa maji Manispaa ya Iringa na kushoto ni Stella
Kiwele Mganga mkuu msaidizi wa Hospitali ya Wilaya Iringa.
Mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 20 na unatarajiwa
kusaidia watu zaidi ya 150.000 katika manispaa hiyo wanaozunguka eneo la
Hospitali.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Teddy Mapunda
akisaini kitabu cha wageni wakati alipowasili hospitalini hapo tayari
kwa ukaguzi wa mradi wa Uvunaji maji unaojengwa katika hospitali hiyo,
kulia ni Mwenyeji wake Stella Kiwele Mganga Mkuu msaidizi wa Hospitali
ya Wilaya Iringa, na kushoto ni Nandi Mwiyombela Meneja wa Miradi
Endelevu na Uwajibikaji.






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)