Waziri
Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Walimu wa
Shule ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro,Sista Martha wakati
akiwasili shuleni hapo.Kulia ni Mke wa, Lowassa,Mama Regina Lowassa na
wa pili (kushoto) ni Mkuu wa Shule hiyo, Sista Dennis
Wanafunzi
wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani
Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha,Waziri Mkuu Mstaafu.
Waziri
Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa
wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya
Mkoani Morogoro.
Waziri
Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista
Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule
hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa
viongozi wa baadaye.
*******************************
Na mwandishi Wetu, Morogoro
Waziri
Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa
bidi ili waweze kuwa viongozi wazuri na tegemezi wa baadaye.
Lowassa,
ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi na viongozi
wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya mtakatifu Anns iliyopo mjini
Morogoro leo.
Baada
ya kutembelea na kujionea mazingira halisi ya shule hiyo, Lowassa
alitoa zawadi ya mipira kwa kila darasa katika shule hiyo, ikiwa ni moja
ya njia ya kuhamasisha michezo mashuleni.
Naye
Mkuu wa shule hiyo, Sister Dennis, pamoja na wanafunzi na watawa
wengine wa shuleni hiyo walimshukuru Lowassa kwa kufanya ziara hiyo
shuleni hapo na kushukuru kwa kuwapatia zawadi ya mipira na kumtakia
afya njema ili aweze kuendelea kuwatumikia watanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)