Hata Madereva waliokuwa wakiendelea na mafunzo ya udereva walifika viwanjani hapo kuwaletea wenzao msosi.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifunua mashine ya king’ola kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo, Kitaifa mkoani Tanga.
Makamu
wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiangalia viatu na kusikiliza maelezo kuhsu utengenezaji wa bidhaa
hiyo kutoka kwa Deogratias John (kushoto) wa
Chuo cha Waleavu cha Usariva Moshi, wakati akitembelea katika mabanda
ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo Kitaifa mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku Galawa. Wa pili (kushoto) ni
Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah Moshi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka
kwa Mkurugenzi na mwasisi wa Chuo cha Gemmologiacal and jewelry Vocation
cha Arusha, Peter Salla, kuhusu matumizi yam awe ya madini, wakati
akitembelea katika mabanda ya maonyesho alipozindua rasmi maadhimisho ya
Wiki ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, yaliyoanza leo, Kitaifa
mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Kapteni Mstaafu, Chiku
Galawa. Wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa VETA, Mhandisi. Zebadiah
Moshi.
Watoto
walioiva katika Sanaa ya kupiga vyombo katika kundi maalum la Chuo cha
VETA, wakitoa burudani kwa kupiga wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu wa
Rais Viwanjani hapo leo, lakini pamoja na udogo wa watoto hawa bado
waliweza kuwashangaza watu waliofika mahala hapo kwa kumudu vyema kupiga
vyombo hivyo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)