Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk.
Mary Nagu akisalimiana na aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na
Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Zhao Zhongqiu leo
ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhongqiu alimtembelea waziri huyo
kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa
nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akisalimiana na Mwakilishi Mkuu
mpya wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania
Lin Zhiyong leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhiyong anachukua
nafasi ya Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk.Mary
Nagu akiongea na ujumbe wa wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu
wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake jijini
Dar es Salaam . Ujumbe huo uliongelea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja
na jinsi ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya
Tanzania na China.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dk.Mary
Nagu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Uchumi
na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea
leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Lin Zhiyong ambaye ni Mwalikishi mpya na kulia ni Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)