MAULIDI YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD KISIWANI TUMBATU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAULIDI YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD KISIWANI TUMBATU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono wananchi waliofika kumpokea wakati alipowasili katika bandari ya Kisiwa cha Tumbatu kuhudhuria katika Sherehe za uzinduzi wa Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W),yaliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani. Tr 21/02/2012 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akifuatana na Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora,pia Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Haji Omar Kheri,pamoja na viongozi wengine wakielekea katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,kuhudhuria katika Sherehe za uzinduzi wa Maulid ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W),mara baada ya kuwasilimkatika kisiwa cha Tumbatu.Tir 21/02/2012
Baadhi ya Akina Mama waliohudhuria katika hafla ya upandishwaji wa Bendera,wakati wa Uzinduzi wa sherehe za Maulidi ya kuzaliwa kwa Nabii Muhammad (S.A.W) akiwa mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,zilizofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tumbatu Gomani. 21/02/2012.
Mamia ya wananchi wa shehia za Tumbatu wakishuhudia upandishwaji wa Bendera wakati wa Uzinduzi wa sherehe za Maulidi ya kuzaliwa kwa Nabii Muhammad (S.A.W),iliyopandishwa na Sheikh Makame Kheir,mbele ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani.
Baadhi ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Tumbatu na Vijiji jirani wakiwa katika Msikiti wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,wakati wa uzinduzi wa Sherehe za Maulidi ya kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) zilizofanyika mwezi 29 mwandamo wa Mfunguo sita,sawana Tarehe 21Feb 2012.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) pamoja na viongozi wengine na Mashekhe mbali mbali walioalikwa katika Sherehe za Uzinduzi wa Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) wakiwa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,yalimofanyika maulidi hayo.
Sheikh Abubakar Said,akisoma Maulid Barzanji Mlango wa Dua,wakati wa Sherehe za Uzinduzi wa Maulidi ya Kuzaliwa Nabii Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Tumbatu Gomani,ambapo waislamu kwa maelfu walihuduria Maulid hayo, yanayosomwa kila mwaka ifikapo mwezi 29 mwadamo Mfunguo sita.(Picha na Ramadhan Othman Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages