Maelfu Wamzika Herbert Aman Mroki Ugweno - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Maelfu Wamzika Herbert Aman Mroki Ugweno

 Waombolezaji wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Herbert Aman Mroki, kuupeleka Makaburini kwaajili ya maziko juzi Jumamosi Februari 18,2012 Ugweno Msangeni.
 Baba mdogo wa marehemu na mzee wa Ikamba Kivunja akiweka shada
 Mamamzazi wa Marehemu akiweka shada la maua
 Mjane wa marehemu akiweka shada la maua katika kaburi la mumewe.
 Watoto wakiweka maua kaburi la baba yao.
 Mr na Mrs Atenaka wakiweka maua katika kaburi la marehemu
 Mjane wa Marehemu (kushoto) akiwa na wakwe zake mama mdogo wa marehemu na mama mzazi wa marehemu.
Naibu Waziri wa Habari,Vijana na Michezo, Dk. Fenela Mkangara akisema neno
---
WASIFU WA MAREHEMU HELBERT AMAN NATHAN MROKI

Marehemu Herbert Aman Nathan Mroki alizaliwa Februari 1,1946 katika kijiji cha Hedaru, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Wakati huo wazazi wake wakiwa wanafanya kazi huko.
Alibatizwa mwaka huohuo 1946 mwezi Aprili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kifula Ugweno.

Marehemu alianza shule ya msingi mwaka 1953 katika shule ya Msingi Hedaru hadi darasa la nne na kuhamia shule ya kati (Middle School) Masumbeni Ugweno hadi aliposoma darasa la tano hadi la nane na kufaulu kwenda Shule ya Sekondari Tanga (Tanga School) ambapo alisoma hapo hadi mwaka 1964 na Mwaka huo huo mwishoni alijiunga na Chuo cha Ushirika Moshi na kufanikiwa kupata Diploma ya Maendeo na Ushirika..

Alifanikiwa kupata ajira yake ya kwanza mwaka 1966 katika Ushirika wa Mount Usambara Cooperative Society akiwa ni Meneja. Mwaka 1970 alikwenda nchini Ujerumani katika jiji la Born kwa mafunzo zaidi na mwaka 1971 alirejea nchini na kuendelea na kazi hadi mwaka 1972 alipoamua kuacha kazi katika Ushirika na kuamua kufanya shughuli zake.

Mwaka 1975 aliamua kurudi tena katika ajira na kuajiriwa Idara ya Biashara za Ndani upande wa RTC na kufanya kazi katika vituo mbalimbali kama Meneja.

Miongoni mwa vituo hivyo ni Bukoba (1975) Karagwe (1977), Same (1982), Rombo (1987) na Lushoto (1991).

Mwaka 1992 aliamua kuacha kazi na kujiunga katika Ujasiriamali ambao aliufanya hadi mwaka 1995 alipoajiriwa tena na Kampuni ya Udalali ya Majenbe Auction Mart “Vijana wa Kazi” akiwa Mwakilishi wa Kanda ya Kaskazini kazi aliyoifanya hadi kifo kinamfika.

Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa wa kiume na Kadhaa wa kike, wajukuu 23 na Kitukuu 1. Marehemu alikuwa akisumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu hadi alipogunduliwa kuwa ana saratani (Kansa). Alianza kupatiwa matibabu na hali yake ilianza kuwa nzuri baada ya upasuaji lakini ghafla hali yake ilibadilika ghafla asubuhi ya Februari 15,2012 na kukimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na hapo alikaa kwa muda wa saa takriban saba na ilipofika saa saba na nusu mchana alifariki dunia.

Shukrani ziwaendee madaktari wote wa Arusha Mt. Meru Hospital, Muhimbili Dar es Salaam na KCMC Moshi. Familia hatuna cha kusema zaidi ya Asante sana na Mungu atawazidishia.

“BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE AMINI”

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages