Makamu
Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF
Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkurugenzi wa habari na haki za
binadamu wa Chama hicho Salim Bimani baada ya kuwasili katika hoteli ya
Mazsons Mjini Zanzibar kwa ajili ya kufungua semina elekezi kwa
wenyeviti na makatibu wa wilaya wa CUF. Katikati ni mwakilishi wa Jimbo
la mgogoni Pemba Aboubakar Khamis Bakar.
Makamu
Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF
Maalim Seif Sharif Hamad akielekea ukumbi wa mkutano katika hoteli ya
Mazsons Mjini Zanzibar kwa ajili ya kufungua semina elekezi kwa
wenyeviti na makatibu wa wilaya wa CUF.Picha na Salmin Said-Ofisi ya
Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
---
Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad
amewataka watendaji wa chama hicho ngazi ya wilaya kufanya kazi kwa
karibu na wanachama ikiwa ni hatua muhimu katika kukijenga chama
chao.Amesema watendaji hao wana nafasi kubwa katika kukijenga na
kukiimarisha chama hicho, ikizingatiwa kuwa wao ndio wenye mawasilianao
ya karibu zaidi na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla.
Maalim
Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ametoa
changamoto hiyo leo huko hoteli ya Mazsons Shangani mjini Zanzibar,
alipokuwa akifungua semina elekezi kwa wenyeviti na makatibu wa wilaya
wa chama hicho, yenye lengo la kujadili juu ya dhana ya utumishi wa
umma.
Amewataka wajumbe wa mkutano huo kuijadili dhana hiyo kwa umakini mkubwa, kwa kuzingatia zaidi maslahi na maendeleo ya chama hicho, sambamba na kuhimiza suala la uwajibikaji kwa viongozi wa ngazi zote za chama.
Semina hiyo imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama hicho wakiwemo wenyeviti na makatibu wa wilaya kutoka wilaya zote za Unguja na Pemba.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)