Mkaguzi
Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga akifungua mkutano wa siku tatu
wa wakaguzi wa ndani wa Halmashauri za Serikali za Mitaa na
Sekretarieti za mikoa jana jijini Dar es salaam . Mkutano huo
uliwajumuisha wakaguzi 165 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara kwa lengo
la kuwaelimisha juu ya miongozo ya ukaguzi wa ndani imetolewa hivi
karibuni ili kuboresha ukuguzi wa ndani utakaoleta matokeo mazuri ya
rasilimali na fedha za wananchi .----
Na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam
Mkaguzi
Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga ameagiza wakaguzi wote wa
ndani kuhakikisha kuwa wanasimamia rasilimali za nchi vizuri kwa niaba
ya wananchi ili miradi ilinganishe na thamani ya fedha iliyoombewa.
Mtonga
alitoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa
ndani wa Halmashauri za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za mikoa jana
jijini Dar es salaam .
Alisema
inasikitisha kuona ubadhirifu wa mali za Serikali kama vile ujenzi wa
madarasa hayakidhi viwango unatokea mita chache toka Ofisi kwa Mkaguzi
wa Ndani au mtaa anaoishi bila kuchukua hatua zinazostahili za kuhakiki
kama kweli mradi huo unalingana na fedha zilizotolewa na Serikali.
Mtonga
aliwaagiza wakaguzi wa ndani kuwa wabunifu ili wawe wasimamizi wazuri
wa rasilimali na fedha umma kwa niaba ya wananchi bila kujali kuwa
wanavifaa vya kutosha au hawana .
Aidha
Mkaguzi Mkuu huyo wa Ndani wa Serikali aliwaonya Wakaguz hao kuepuka
tabia ya Ushirikiano na mitandao inayowafanya kikiuka sheria na taratibu
za fedha ambazo ndio zinaweza kusababisha kutoa taarifa zisizokuwa za
sahihi za ukaguzi wa ndani na hivyo kusababisha upotevu wa fedha za
umma.
Alisema
kuwa inasikitisha kuona kuwa inatokea tukio kama la Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu ambalo lilitokana na ukaguzi maalumu wa mwaka
2007/2008 hadi 2009/2010 wakati Mkaguzi wa Ndani yupo .
Katika
hatua nyingine Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mtonga alisema kuwa
Ofisi yake inaandaa Mwongozo utakaowasaidia wakaguzi wa Ndani kukaguzi
bajeti na kuangalia utekelezaji wake.
Hatua
hiyo inalenga kuhakikisha kunakuwepo kwa uwazi na uwajibikaji kwa
watendaji ili mwananchi ajue bajeti inakwendaji na kitu gani kinatakiwa
kufanyika ili kumletea maendeleo kulingana na mapendekezo ya vipaumbele
vilivyoombewa fedha.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)