Waziri
wa Fedha Mustapha Mkulo akitoa maelezo ya awali kuhusu maendeleo ya
kazi za maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyopangwa kufanyika
nchini wakati wa semina kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi iliyofanyika
jana katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma,Hata hivyo waziri
Mkulo amefafanua kuwa serikali itahakikisha kuwa sensa hiyo inafanyika
kama ilivyopangwa kwa ubora na ufanisi ikilinganisha na sensa
zilizopita.
Manaibu
waziri wa Fedha Gregory Theu (kushoto) na Pereira Silima(kulia)
wakifuatilia masuala mbalimbali kuhusu Sensa ya watu na makazi
itakayofanyika mwaka huu wakati semina iliyowahusisha wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jamii na Kamati ya Fedha na Uchumi jana mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)