Mwalimu
mkuu wa shule ya sekondari ya Yaeda Ampa Mary Genda na wanafunzi wa
shule hiyo wakipokea vitabu toka kwa Afisa uhusiano wa Airtel Jane
Matinde vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule
za sekondari nne za mkoa wa Manyara ambazo ni Yaeda Ampa, Yaeda Chii ,
Naberera na Merelani B.w Mkapa chini ya mpango wake wa shule yetu
halfa iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii.
Afisa
Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ,Jane Matinde
akikabidhi vitabu kwa Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu Mikaeli
Hadu ,kwa niaba ya shule nne za sekondari zilizokabidhiwa vitabu hivyo
vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila shuke,shule hizo ni
Yaeda Ampa, Yaeda Chii , Naberera na Merelani B.w Mkapa,Mkoani Manyara
(katikati )ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya
Mbulu Bw.Harry Sinjela.
Wanafunzi
, walimu ,wafanyakazi wa Airtel na viongozi mbalimbali wa halmashauri
ya wilaya ya mbulu mkoani Manyara wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya Airtel kukabithi vitabu kwa shule 4 za sekondari zilizopo
mkoani hapa, kila shule imepata vitabu vya thamani ya shilling milioni
moja. Walikaa kutoka kushoto ni Afisa wa uhusiano wa Airtel Jane
Matinde Akifatiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya mbulu
Bwana Harry Sinjela, Afisa Elimu sekondari wa wilaya ya Mbulu Mikaeli
Hadu na diwani wa kata ya Yaeda Ampa Bw Marcel Malley.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)