MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAFANYA UKAGUZI WA VITAMBULISHO KWA WANACHAMA WAKE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAFANYA UKAGUZI WA VITAMBULISHO KWA WANACHAMA WAKE

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya bwn. Immanuel Humba akifafanua mbele ya wanahabari  kuhusu zoezi la ukaguzi wa vitambulisho kwa wanachama wake kwenye hospitali na vituo mbalimbali vya kutolea huduma,kumekuwepo kwa matumizi yasiyo sahihi kwa wanachama wachache wasio waaminifu,amewataadharisha wanachama watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mkurugenz wa Operesheni bwn. Eugin Mikongoti akiwaeleza waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa zoezi la ukaguzi wa vitambulisho vya wanachama wa NHIF, ambapo amewataka wanachama,waajiri na watoa huduma kulipokea kwa mtazamo chanya na kutoa ushirikiano kwani una lengo la kudhibiti wanachama wasio waaminifu ambao wana lengo la kudhoofisha malengo ya mfuko huo.kushoto mwisho mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF bwn Immanuel Humba,na katikati ni mkurugenizi wa fedha na iwekezaji bwn. Deusdedit Rutazaa.
Na Grace Michael

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages