Vijana waliomakatwa na meno ya Tembo waliokamatwa jana Mkoani
Morogoro ambao walitambulikwa ka majina yao,Erick Kiari (kushoto) mwenye
miaka 23, Abel Adrian (katikati) pia anamiaka 23 na Anaheri Mkindi
ambaye umri wake ni miaka 17 wakiwa chini ya ulinzi katika kituo cha
polisi mkoa wa Morogoro mara baada ya kukamatwa na meno ya tembo vipande
51 wakati wakisafiri kutoka mkoa wa Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam
kwa kutumia Gari yenye Namba DFP 3468 ambayo inadaiwa kuwa ilibandikwa
tu na si Nambari zake za usajili na ilikuwa ni gari ya Mtu
binafsi.Watuhumiwa hawa wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kesho
jumatatu ili kujibu mashtaka yao.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)