Aba
Seduu wa kampuni ya Scanard Tanzania akielezea jinsi ambavyo Coca-Cola
teen parties zitakavyoendeshwa nchi nzima kuanzia kesho Jumamosi
Februari 11 ambapo burudani hizo za vijana zitazinduliwa rasmi jijini
Mwanza na kutumbuizwa na mwanamuziki nyota wa kizazi kipya Mwasiti
Almasi. Lengo ni kuwapa vijana fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika
mambo mbali mbali kama vile burudani. Kulia ni Meneja Masoko wa
Coca-Cola Tanzania Salome Mabirizi.
Meneja
Masoko wa Coca-Cola Tanzania Salome Mabirizi akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari kuhusu Coca-Cola ‘teen parties’ au Waka Waka na
Coca-Cola inayojumuisha vijana wenye umri kati ya miaka 13 na 19. Lengo
ni kuwapa fursa vijana kuonyesha ubunifu wao katika mambo mbali mbali
kama vile burudani. Uzinduzi rasmi wa teen parties unafanyika Mwanza
kesho Jumamosi Februari 11 ambapo mwanamuziki nyota wa kizazi kipya
Mwasiti Almasi atatumbuiza. Kushoto ni Aba Seduu wa Scanard ambayo ndiyo
kampuni inayoratibu teen parties.Picha Na Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)