KUFA KWA MUZIKI WA BONGO KUNACHANGIWA NA BAADHI YA WASANII WAKUBWA WA HAPA NYUMBANI.
Tulitegemea
kwa wasanii wakubwa kama Ambwene Yesaya A.Y kama anavyofahamika
kwa mashabiki wengi wa muziki, angekuwa ni mfano wa kuigwa na wanamuziki
chipukizi hapa nchini,ila baadala yake ameonekana kutokuwa na
discipline na kikwazo kikubwa cha kukua kwa muziki wa reggae na ragga
hapa nchini.
Sisi
kama Jahson na Susu hatuwezi kujifunza lolote kutoka kwa msanii huyo
(A.Y) kwa sababu amekuwa ni mtu alionyesha utovu wa nidhamu ya hali ya
juu mara kadha wa kadha mfano.
Wengi
tunamjua A.Y kama msanii wa Hip Hop lakini mwaka 2010 aliwai
kushindania tunzo ya mwanamuziki bora wa reggae na hatimaye kupata tunzo
hiyo na kuichukua kwa mbwebwe zote na Pia mwaka huu 2012 amewekwa
kwenye category ya ragga na nina imani atapata tu tunzo hiyo kutokana
ma madhaifu yaliyopo katika uandaaji wa tunzo hizo za Kilimanjaro music
award.
Bushoke alikuwa mfano mzuri sana wa kuigwa alipopewa tunzo ambayo hakustahili na kuikataa je A.Y kwa nini alikubali tunzo hiyo? Na ki ukweli haikumstahili
Ki
ukweli wasanii kama A.Y wanatuvunja moyo sana sisi wasanii ambao
tunaofanya muziki huo pamoja na mashabiki wa muziki huo wa reggae na
ragga na kwa taharifa yake tu bwana AY asijidanganye kwa wingi ama
uchache wa kura hizo anazopata katika kinyang’anyilo hicho ,asidhani
kama anapigiwa na mashabiki wa Reggae na ragga,no huo ni uongo mtupu ni
mashabiki wake wa hip hop ndo wanaomuwezesha so anawakanganya wapenzi
wake kiukweli.
Sisi
kama washikadau wakubwa wa muziki huu wa Ragga na Reggae
tumesikitishwa sana kwa mapungufu makubwa ya msanii huyo AY kuzidi
kukumbatia ujinga unaofanyika kila mwaka sijui anataka tujifunze nini
msanii huyo bwana Ambene yesaya.
Atumchukii AY hapana ila tunajalibu kuweka mambo wazi na kutoruhusu ujinga huu kuendelea maana kunawakati ataimba Taarabu na na Bolingo na watamuweka kwenye category hiyo na atachukuwa.inawezekana kabisa akawa anauwa muziki wake ama anawagawanya mashabiki wake kwa kutotulia kwenye style ya muziki wake,na kuwa kama Inzi anavyotua mara kwenye embe bovu mara kwenye kidonda mara jalalani,atumuelewi bwana A.Y.
Tungependa
washikadau wa wakubwa wa muziki huu walione kama hili ni tatizo na
walikemee kwa nguvu zote ili Tanzania iwe na ukomavu wa muziki huu
tofauti na hapo tutakuwa tunapiga kwata bila kusonga mbele.
Sisi tumeshafanya nyimbo kama Heat na Show me some love ambazo zimefanya wema katika vituo mbalimbali lakini tumeenguliwa kwenye tunzo hizo hii inakatisha tamaaaa sana,lakini sisi hatutokata tama na wala haitufundishi uonga wa kupigana na kitu ambacho tunaamini tunakifanya vema kabisa japo kuna wasanii wengi wakali waliamua kuachana na muziki kwa ajiri ya mambo ya kinyama kama haya.Shabiki wetu jaribu kuingia kwenye youtube na usearch Jahson & Susu ama Jahson Tanzania alafu utoe coment je tunastahili kunyimwa tunzo hizo?
Asanteni ni sisi Jahson na Susu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)