Familia ya Kusaga inawaomba
watanzania wote walioko Marekani na hasa eneo la Washington DC na
vitongoji vyake kushirikiana nao katika harambee (fundraising) ili
kupata pesa ya mazishi ya mtanzania mwenzetu Christavina Kusaga Cryor
aliyefariki February 7, 2012 kwa saratani ya utumbo (Colon Cancer)
Marehemu alikuwa akiishi Landover, MD. Ameacha mume na watoto
wawili- mvulana wa miaka 4 na msichana wa miaka 2. Alikuwa akisumbuliwa
na cancer ya utumbo.
Tafadhali fika tushirikiane kumsaidia mume wake na watoto na
familia wamzike mpendwa wao. Jumla ya gharama za mazishi ni $11,000, na
mpaka sasa ni $2,000 tu imepatikana. Tunashukuru kwa waliokwisha
saidia.
Harambee itakuwa Jumapili February 12, 2012, kuanzia saa 8.30 mchana (2.30pm).Anuani ni: 3621 Campus Drive, College Park, MD 20740.
Kwa wale wa mbali au wasioweza kuhudhuria tafadhali tusaidie
mchango wako kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing
# 255071981. Tafadhali eneza habari hii kwa ndugu na marafiki wote.
Asanteni sana kwa ushirikiano wenu katika wakati huu mgumu.
Kwa habari zaidi mpigie: Magoma (202.607.1976); Adelaida
(240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile (240.938.3177); Teddy
(301.25441696); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au
Rebecca (202.580.4648). **********R.I.P Christavina*************
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)