TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
(TANZANIA COMMISSION FOR UNIVERSITIES – TCU)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UENDESHWAJI WA UDAHILI - ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013
UTANGULIZI
Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (‘Tanzania Commission for Universities’-TCU)
ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (‘National Council
for Technical Education’ - NACTE) pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
Elimu ya Juu (Higher Education Students Loans Board) inapenda kuutarifu
umma kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka wa
masomo 2012/2013 kupitia mifumo ya “Pre-entry”, “Mature Age Entry”,
“Equivalent Qualifications” na mfumo wa pamoja wa udahili (‘Central
Admission System’) na utaratibu wa mikopo kama ifuatavyo:
MFUMO WA UDAHILI KUANZIA MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za “Pre-entry” na “Mature Age Entry”
Kuanzia
mwaka huu 2012, vyuo vyote vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya awali
kabla ya mwombaji kustahili kudahiliwa ili kuweza kujiunga na programu
za elimu ya juu (pre-entry programmes) pamoja na kuendesha mitihani ya
kupitia mfumo wa “Mature Age Entry” vinatakiwa kuwasilisha programu hizo
Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
kwa uhakiki na kupata kibali. Programu hizo ni lazima ziendeshwe kwa
muda wa mwaka mmoja. Hali kadhalika kwa upande wa mitihani kupitia mfumo
wa mature entry, Tume kwa ushirikiano na Baraza, kwa pamoja wataandaa
na kuratibu utaratibu wa mitihani katika vituo maalum kikanda ili vyeti
vitakavyotolewa viwe na ulinganifu unaostahili na hatimaye kuweza
kutumika katika udahili wa sifa linganishi katika vyuo mbalimbali.
Vyuo
vinatakiwa kuandaa programu za mifumo ya “Pre-entry” na “Mature Age
Entry” na kuziwasilisha Tume na Baraza ili zihakikiwe kwani mwaka wa
masomo kwa kusudi hili utaanza mwezi Agosti 2012/2013. Kwa utaratibu
huu, watakaofanya mafunzo hayo watatakiwa kufanya mitihani yao na
kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Kwa taarifa hii, mwaka 2012/13 hakutakuwapo na udahili wa wanafunzi kwa mfumo wa “Pre-Entry” na “Mature Age Entry”.
1.2 Utaratibu wa Udahili Kupitia Mfumo wa Pamoja (Central Admission System)
Waombaji
watakaopitia mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) wamegawanyika katika
makundi manne, ambapo waombaji wa kundi (i), (ii) na (iii) watatambuliwa
kama “Direct Applicants” na kundi (iv) watatambuliwa kama “Indirect
Applicants”
Waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita katika kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka huu.
Waliohitimu
mafunzo ya diploma ya elimu ya ufundi (NTA level 6) kutoka vyuo
vinavyotambulika na NACTE miaka miwili iliyopita pamoja na wale
watakaohitimu mwaka huu;
Waliohitimu
mafunzo ya Diploma ya Ualimu (kutoka vyuo vinavyotambulika) katika
kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na wale watakaohitimu mwaka
huu.
Waombaji
ambao sio wa moja kwa moja (Indirect Applicants) ni wote waliohitimu
kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level 6) na Diploma ya
Ualimu katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita (kuanzia 2009
kurudi nyuma).
1.2 Waombaji Watakaowasilisha Maombi yao Moja kwa Moja Vyuoni
Waombaji
watakaowasilisha maombi kupitia vyuo husika ni wenye sifa linganishi
(Equivalent Qualifications) yaani wenye vyeti vya Astashahada na Diploma
ambazo hazitambuliwi moja kwa moja na NACTE. Ili kukamilisha udahili,
wanashauriwa kuwasiliana na NACTE ili vyeti vyao vitambuliwe na
kusajiliwa kabla udahili haujaanza.
Vyuo
vinavyofundisha programu mbalimbali katika ngazi ya Astashahada na
Diploma ambavyo havina usajili wa NACTE/NECTA vinatakiwa kuwasilisha
matokeo ya wanafunzi wao NACTE haraka iwezekanavyo ili matokeo hayo
yaweze kutumika katika utambuzi wa vyeti vya wanafunzi husika.
MUDA WA UDAHILI KWA MAKUNDI MBALIMBALI
Muda wa maombi wa kuwasilisha maombi ya udahili kwenye CAS umegawanyika katika makundi matatu kama ifuatavyo:
Kundi la Kwanza – (1 Aprili mpaka 30 Aprili 2012)
Waombaji
wote waliomaliza kidato cha sita, Diploma ya Elimu ya Ufundi (NTA level
6), na Diploma ya Ualimu kuanzia mwaka 2011 kurudi nyuma wataanza
kuomba udahili kuanzia Aprili 1, 2012 hadi 30 Aprili 2012.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)