KLABU ya soka ya Simba inatarajiwa kuzindua Simba Tv siku ya Ijumaa
katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katika jengo la Benjamin Mkapa,
katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Msemaji wa Simba Ezeckiel Kamwaga amesema leo kwamba, Simba Tv itakuwa
ikirushwa katika kituo cha Televisheni cha Clouds Fm ambapo itakuwa
ikizungumzia masuala mbalimbali yahusuyo klabu hiyo.
Alisema uzinduzi huo utakaokuwa kwa wageni waalikwa tu huku kwa
wengine watakaotaka kuhudhuria watapaswa kulipa shilingi 70,000 kwa
kila mtu, utaambatana na burudani mbalimbali sambamba kuonyeshwa
historia ya Simba.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)