MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MSHUJAA WA VITA VYA MAJIMAJI MJINI SONGEA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MSHUJAA WA VITA VYA MAJIMAJI MJINI SONGEA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiongea wakati wa Sherehe za kumbukumbu ya Mashujaa wa vita ya Majimaji iliyoadhimishwa jana mjini songea.Kushoto ni Kkatibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi na Kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel Zullu.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanal Mstaafu Joseph Simbakalia akiongea na wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji yaliyofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini humo.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi. Maimuna Tarishi na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi akiongea na wakazi wa manispaa ya songea kwenye maadhimisho ya kumbukmbu ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini songea jana.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu na kulia ni Chifu wa Wangoni,Ndg. Emmanuel Zullu.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu akiweka ngao na mkuki katika mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini songea
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Bi Maimuna Tarishi,Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoani Ruvuma,Alhaji Mustafa Songambele na Mkuu wa Zamani wa Mkoa wa Ruvuma,Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo wakiinua mikono juu ikiwa ni ishara ya kuomba dua kwa Mashujaa wa Vita ya Majimaji wakati wa maadhimisho ya Mashujaa hao mjini songea jana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages