SIKU YA SHERIA NCHINI MKOANI RUKWA YAFANA HAPO JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SIKU YA SHERIA NCHINI MKOANI RUKWA YAFANA HAPO JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akitoa neno lake la shukrani katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika jana katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G.K. Rwakibarila na Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda hiyo.
Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Kanali John Mzurikwao, Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G. K. Rwakibarilla, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya, Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Sumbawanga Prosper Rwegerera wakiangalia Kwanya iliyokuwa ikitumbuiza katika Sherehe za Siku ya Sheria Nchini jana.
Mhe. Jaji Mfawaidhi G. K. Rwakibarila akikagua Gwaride hilo.
Mhe. Jaji Mfawidhi akiteta jambo na wenzake mara baada ya kukagua Gwaride la heshima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakijumuika kwenye kwaya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akijumuika kupanda Mti katika eneo la Mahakama hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Sheria .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, katibu wake Frank Mateny (kushoto), Afisa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa George Kiria na Mpelelezi Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Rukwa wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakisubiri kuanza kusikiliza mashauri yaliyopangwa kusikilizwa katika mahakama hiyo yaliyombatana na maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages